LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kituo cha kukuza biashara za wajasiriamali chazinduliwa jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amezindua kituo cha kuendeleza ukuaji wa biashara za wajasiriamali kupitia shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) chini ya mradi wa SIDO TLED HUB.

Mongella alifanya uzinduzi huo Januari 24, 2020 katika viunga vya ofisi za SIDO Nyakato jijini Mwanza na kubainisha kwamba serikali mkoani Mwanza iko tayari kutoa ardhi kwa ajili ya shughuli za viwanda vidogo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkurugenzi Mkuu SIDO, alisema Profesa Sylvester Mpanduji akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Meneja SIDO Mkoa Mwanza, Bakari Songwe akitoa salamu zake kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Mariam Munanka akitoa salamu zake kwenye uzinduzi huo.
 Rais wa chama cha wafanyabiashara, viwanda na kilimo TCCIA, Paul Koyi akizungumza kwenye ufunguzi huo.
Mkurugenzi Mkazi Shirika la VSO, Dawn Hoyle akitoa salamu zake kwenye mkutano huo.
Mwakilishi Ubalozi wa Canada nchini Tanzania, Christopher Duguid akitoa salamu zake kwenye uzinduzi huo.
Mwakilishi shirika la Africa CUSO International, David Forest akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mwakilishi Mkazi Shirika la Africa CUSO International, Romanus Mtunge akitoa salamu zake kwenye uzinduzi huo.
 Wadau mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Wadau wakifuatilia hafla hiyo.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Mwanza Quality Wines inayotengeneza mvinyo wa matunda (Power Banana), Leopord Lema (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusiana na bidhaa hiyo baada ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) kutembelea mabanda ya wajasiriamali mbalimbali waliohudhuria halfa hiyo.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) akifurahia jambo baada ya kutembelea banda la kampuni ya Mwanza Quality Wines.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.