LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanafunzi wa Vyuo Mwanza wamepwa mafunzo "kukataa Rushwa ya ngono"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa Wilaya Ilemela mkoani Mwanza, Dkt. Severine Lalika (kulia) akifungua mafunzo kwa wanafunzi wa vyuo vya SAUT Malimbe, Butimba TCC pamoja na CUHAS Bugando yaliyoandaliwa na TAKUKURU Mkoa Mwanza ili kuwajengea uwezo kukataa Rushwa ya ngono.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa Mwanza, Daud Ndyamukama akieleza umuhimu wa mafunzo hayo.
Wanafunzi wa vyuo mbalimbali jijini Mwanza wakifuatilia mafunzo ya kukomesha rushwa ya ngono yaliyoandaliwa na TAKUKURU Mkoa Mwanza.
Viongozi mbalimbali akiwemo mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Ilemela, Dkt. Severine Lalila (wa tatu).
"Vunja Ukimya...Kataa Rushwa ya Ngono".
Wanafunzi wa vyuo jijini Mwanza wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo kukataa rushwa ya ngono.
Wanafunzi wa vyuo mbalimbali jijini Mwanza wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo kupinga rushwa ya ngono vyuoni.
Washiriki wa mafunzo hayo pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Wanafunzi wa vyuo jijini Mwanza walioshiriki mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya Ilemela, Dkt. Severine Lalika (wa tano waliokaa).
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa Mwanza imetoa mafunzo kwa wanafunzi wa vyuo vya SAUT Malime, CUHAS Bugando pamoja na Butimba TCC ili kuwajengea uwezo kukataa rushwa ya ngono vyuoni.

Mafunzo hayo yamefanyika Juni 28, 2020 katika Chuo cha SAUT yakiwakutanisha wanafunzi mbalimbali wakiwemo wanauounda Klabu za wapinga rushwa vyuoni huku msisitizo mkubwa ukitolewa kwa wanafunzi hao kuvunja ukimya na kutonyamazia rushwa ya ngono vyuoni.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo, Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa Mwanza Daud Ndyamukama alisema licha ya kuwa rushwa ya ngono ni kosa la jinai lakini pia ni kikwazo cha maendeleo ya mtu binafsi na nchi pia.

“Rushwa ya ngono ni tatizo ambalo linakwamisha maendeleo ya mwanafunzi, pia inaweza kumnyika haki mwanafunzi pale anapokataa na hivyo kutatiza maendeleo yake ya kitaaluma. Lakini pia rushwa ya ngono ikikubalika matokeo yake ni kupata wahitimu wasio na sifa” alieleza Ndyamukama akiwataka wanafunzi hayo kutonyamazia rushwa ya ngono.

Awali akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya Ilemela Dkt. Severine Lalika aliwataka wahadhili na wanafunzi wa vyuo kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha wanapinga rushwa ya ngono akisema ‘digrii za chupi’ siyo dili kwa sasa kwani zinawaondolea utu wanafunzi wa kike na wa kiume.

Nao baadhi ya wanafunzi walioshiriki mafunzi hayo akiwemo Adson Scotty kutoka Chuo cha CUHAS Bugando walisema rushwa ya ngono vyuoni ina athari kubwa kitaaluma kwa sababu inaondoa ari ya wanafunzi kujifunza na kutegemea msaada kutoka kwa wakufunzi.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.