LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biteko awashukuru wananchi wa Bukombe “ahimiza Uzalendo”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Jimbo la Nyanza Gold Belt Field, Enock Sando (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) zawadi ya vitabu vya dini wakati wa ibada ya kilele cha makambi ya Kanisa la SDA Maganzo wilayani Bukombe, Jumamosi Julai 04, 2020. Katikati ni Mchungaji wa Kanisa la SDA Maganzo, Godwin Bitwaiki.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akiteta jambo na Mchungaji wa Kanisa la SDA Maganzo lililopo wilayani Bukombe, Godwin Bitwaiki (kulia) wakati wa kilele cha ibada ya makambi yaliyofanyika kanisani hapo kuanzia Juni 28, 2020.
Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Madini, Doto Biteko wakiwa kwenye ibada hiyo iliyoambatana na harambee ya ujenzi wa nyumba ya Mchungaji wa Kanisa la SDA wilayani Bukombe.
 Waamini mbalimbali wa Kanisa la Waadventista Wasabato wakifuatilia ibada ya kilele cha makambi (Mungu Kwanza) katika Kanisa la SDA Maganzo.
Waziri wa Madini, Doto Biteko amewashukuru wananchi wa jimbo la Bukombe mkoani Geita kwa heshima na ushirikiano waliompa katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake katika nafasi ya ubunge.

Biteko ametoa shukurani hizo Jumamosi Julai 04, 2020 wakati akitoa salamu kwenye ibada ya kilele cha makambi ya Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Maganzo wilayani humo iliyoambatana na harambee aliyoiongoza ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mchungaji.

Aidha Biteko ametumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi wa Bukombe kuendelea kuiombea nchi pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aendelee kuwahudumia watanzania na kuivusha nchi kupitia mambo makubwa ambayo yamefanyika.

Naye Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la "Nyanza Gold Belt Field", Enock Sando amemuombea Waziri Biteko Baraka na Utumishi uliotukuka huku akimshukuru kwa kushiriki ibada hiyo pamoja na sadaka aliyoitoa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mchungaji.
Tazama BMG ONLINE V hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.