LIVE STREAM ADS

Header Ads

Soko alisaka Jimbo la Urambo mkoani Tabora

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mmiliki wa Shule za Santa Maria na Santa Louis, Emmanuel Soko (kulia) amechukua fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo ya Urambo mkoani Tabora kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akichukua fomu hiyo, Soko amesema yuko tayari kuwatumikia  wananchi wa jimbo la Urambo kwa kuwa anatambua changamoto zao na namna atakavyoshirikiana nao katika kuzitatua na hatimae kuhakikisha Urambo inasonga mbele kimaendeleo. 

Soko amekuwa mstari wa mbele kwenye kuchochea maendeleo ya jimbo la Urambo pamoja na kuwaleta pamoja wana Urambo ambapo pia amekuwa kada wa muda mrefu ndani ya CCM na Jumatano April 15, 2020 ameamua kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama  chake kupeperusha bendera ya ubunge katika jimbo hilo.
#BMGHabari

No comments:

Powered by Blogger.