MAJALIWA AWEKA REKODI MWANZA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amefika katika visiwa vidogo vya Irugwa na Ghana katika Wilaya ya Ukerewe (ambayo pia ni kisiwa) mkoani Mwanza kuwaombea kura wagombea wa chama hicho.
Majaliwa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Tanzania amekuwa kiongozi wa kwanza wa kitaifa kufika katika visiwa hivyo tangu miaka na mikaka visiwa hivyo vigundulike.
Akiwa katika kisiwa cha Irugwa, Majaliwa aliahidi kuwa Serikali itajenga Kituo cha Afya kisiwani hapo, kuboresha usafiri wa majini kwa kujenga kivuko pamoja na kununua boti ya spidi ili kuimarisha ulinzi kwa wakazi wa kisiwa hicho.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa (kulia) akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili katika Kisiwa cha Irugwa wilayani Ukerewe.
Diwani mteule wa Viti Maalum (CCM) Kaya ya Irugwa wilayani Ukerewe akiwaombea kura wagombea wa chama hicho. Kulia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa.
Mgombea udiwani Kata ya Irugwa wilayani Ukerewe (kushoto) akiomba kura mbele ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa (kulia).
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa (kulia) akimuombea kura mgombea ubunge jimbo la Ukerewe (kushoto) katika Kisiwa cha Irugwa.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa akionyesha Ilani ya Uchaguzi iliyotekelezwa na Serikali kwa mwaka 2015/20.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa akionyesha Ilani ya Uchaguzi kwa mwaka 2020/25 na kuwaeleza wananchi mambo yaliyoandikwa kwenye Ilani hiyo.
Mmoja wa wakazi wa kisiwa cha Irugwa wilayani Ukerewe akisoma ahadi za zilizoandikwa kwenye Ilani ya CCM kwa mwaka 2020/25 zinazowagusa moja kwa moja ikiwemo ujenzi wa meli na vivuko. Kulia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa ambapo aliwahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM ili wakakamilishe kazi ya kuwaletea maendeleo.
Wakazi wa Irugwa wakifuatilia Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu ambapo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa aliwanadi wagombea wa CCM na kuwaombea kura.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mwanza, Dkt. Antony Diallo akiwaombea kura wagombea wa chama hicho.
Wakazi wa kisiwa cha Iugwa (kushoto) wakimkabidhi Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa kamba kama ishara ya kupokea zawadi ya ng'ombe mmoja waliyemzawadia mgombea wa urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli.
Zawadi ya ng'ombe iliyotolewa na wakazi wa Irugwa kwa mgombea urais wa CCM, Dkt. John Magufuli ilikabidhiwa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Irugwa na hapa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa anakabidhi kamba kwa kiongozi wa wanafunzi wa Shule hiyo kama ishara ya kupokea ng'ombe hiyo.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini
SOMA>>> Habari zaidi
No comments: