LIVE STREAM ADS

Header Ads

Billy Kym: Daktari aliyejikita kwenye muziki

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Kutana na daktari ambaye ana mapenzi zaidi na muziki, anaitwa Billy Kym kutoka nchini Kenya ambaye amekuwa akipata taaluma yake ya udaktari huko nchini Finland kwa miaka kadhaa sasa. 

Billy Kym ambaye licha ya kutingwa na kazi pamoja na masomo, muziki ni moja ya jambo ambalo amehakikisha analipatia muda zaidi ili kuweza kufanikisha ndoto yake. 

Billy kym mpaka sasa amefanikiwa kuchia kazi kadhaa ikiwemo Apologize, Queen, Medication, First Time na hivi sasa ameachia rasmi wimbo wake mpya uitwao Same Page ukiwa umetayarishwa chini ya Richmind Imaging na kutengenezwa na Henzov pamoja na Ernest Canto ambapo video nzima imefanyikia huko huko nchini Finland. 

Unaweza kutazama video hiyo hapa chini ambapo pia unaweza kuwa karibu na Billy Kym kwa kumfuata kupitia ukurasa wake wa Instagram @billykym1
Imeandaliwa na Natty E Brandy

No comments:

Powered by Blogger.