LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge wa Butiama akabidhi jezi kwa timu zinazoshiriki 'Sagini Cup 2021'

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Timu 18 zinazoshiriki mashindano ya soka ya Sagini Cup 2021 katika Wilaya ya Butiama mkoani Mara zimekabidhiwa jezi 270 zenye thamani ya shilingi milioni 1.8 (Tsh. 1,806,400/=).

Akizungumza kwa niaba ya mbunge wa Jimbo la Butiama Jumanne Sagini wakati wa kukabidhi jezi kwa viongozi wa timu kwa kata zote, Jumapili Malima amesema kuwa mbunge ni mpenda michezo amekusudia kuifanya michezo kama ajira kwa vijana na sasa anatekeleza kile alichoahidi.
"Mbunge wetu ni mtu vitendo tumeona mengi aliyofanya kwa muda mfupi akiwa jimboni akitekeleza ahadi zake, hivyo niwaombe viongozi wa timu shiriki kuhakikisha jezi mlizopokea zinatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa pia kila mchezaji awe nayo awapo uwanjani," amesema Malima.

Pia Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Butiama Msoka Msoka ameishukuru Ofisi ya Mbunge kwa kutoa jezi na kuhahidi kama kiongozi atahakikisha zinatumika kwa ajili ya mashindano hayo na si vinginevyo.
Mmoja kati ya waratibu wa mashindano ya Sagini Cup Changalawe Changalawe amesema kuwa lengo la mashindano hayo yatadumisha amani na upendo na kurudisha nidhamu na heshima kwa vijana walioko mtaani.

Akiongea kwa niaba ya waliopokea jezi, Shija Rashid ambaye ni Kocha wa Timu ya Kata ya Kukirango FC amemshukuru Mbunge kwa moyo wa kipekee wa kuamua kuwakomboa vijana kupitia michezo mbalimbali ikiwemo soka na kurudisha heshima ya Butiama kwani kufanya hivyo ni kumuenzi Hayati Baba wa wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

No comments:

Powered by Blogger.