LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ni Simba SC kwa mara nyingine, yagonga vichwa vya habari

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mabingwa watetezi wa soka nchini Tanzania, Simba SC wamepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Gwambina FC katika uwanja wa Gwambina Wilaya Misungwi mkoani Mwanza.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, beki wa kushoto na Nahodha Msaidizi, Mohammed Hussein 'Tshabalala' aliyefunga dakika ya 29 kwa shuti la umbali wa mita 35 baada ya pasi ya kiungo Muzamil Yassin.

Kwa ushindi huo wa jumamosi Aprili 24, 2021, Simba SC inafikisha pointi 58 baada ya kucheza mechi 24 ikiwazidi pointi moja vigogo Yanga SC ambao pia wamecheza mechi 26.

Tshabalala anafunga bao hilo siku mbili tu baada ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumia klabu hiyo hadi mwaka 2024.
Chanzo>>> Bin Zubery Blog

No comments:

Powered by Blogger.