LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wafanyakazi Mradi wa Maji Musoma wagoma

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Rebecca Luzunya, Mara
Wafanyakazi 100 wa mradi wa maji wa Mgango-Kiabakari uliopo katika Halmashauri ya Musoma mkoani Mara wamegoma kufanyakazi kwa muda wakishinika kulipwa stahiki zao na kampuni ya Yun Constraction kutoka nchini Lethoto inayotekeleza mradi huo wa maji.

Wafanyakazi hao wamesema kuwa wamekuwa wakikutana na changamoto ya kukatwa fedha katika mishahara yao na mwajiri wao bila makubaliano yoyote ya kisheria.

Kazimiri Mikaeli mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo amesema kuwa wameanza kukutana na changamoto kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita kwa kukatwa fedha zao ambazo zinadaiwa kuwa ni za mafao ya NSSF bila ya kujaza mikataba yoyote kitu ambacho hawakubaliani nacho.

"Tumekuwa tukikatwa fedha zetu bila utaratibu wowote kutoka kwa bosi wetu, hiki kitu sisi kinatuumiza kwa sababu tunafanya kazi na kutegemea kupata stahiki zetu badala yake wanakata hela zetu bila kufuata sheria zozote" alieleza Kazimiri.

|Naye Katibu wa Chama cha Wafanyakazi (TUICO) Mkoa wa Mara, Kanuti Magashi alifika katika eneo hilo na kukutana na changamoto hiyo na kuwataka wafanyakizi hao kwa kushirikiana na viongozi wa kampuni hiyo kupata mikataba na kuipitia ili kujiridhisha.

"Mnatakiwa mshirikiane na mwajiri wenu ili muweze kupitia mikataba yenu kwa usahihi ili kuondokana na changamoto mbalimbali, pia nimewaagiza kufikia jumatatu muwe mmeshapata taarifa za uhakika zinazoelezea makato yenu kupelekwa NSSF, mpate na vitambulisho" alisema Magashi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt.Vicent Naano alitoa maagizo kwa Idara ya Kazi pamoja na NSSF kuhakikisha wanafanya kazi zao ipasavyo kwa kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ili wafanyakazi waweze kupata haki zao kulingana na sheria.

Naano aliwataka wafanyakazi kufanya kazi kwa umakini na kuacha udokozi, uvivu na maneno ya chinichini tabia ambazo zimekuwa zikiripotiwa kwake kutoka kwa mwajiri wao.

No comments:

Powered by Blogger.