LIVE STREAM ADS

Header Ads

TARURA yatambulisha mfumo mpya wa kulipia maegesho jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umeanzisha mfumo mpya wa kielektroniki wa ukusanyaji ushuru wa maegesho ujulikanao kama TARURA e-Revenue Management Information System (TeRMIS) ili kuboresha ukusanyaji wa mapato na kuondoa changamoto zilizokuwepo awali ikiwemo mlipaji kutopata namba ya malipo kwa wakati.

Akizungumza wakati wa kuutambulisha mfumo huo, Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amesema utaongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali yatakayosaidia kuboresha miundombinu ya barabara huku mtumiaji wa maegesho akichagua afanya malipo kwa saa, masaa, siku, wiki ama mwezi.

Naye Afisa TEHAMA TARURA, Shadrack Mahenge amesema mfumo huo wa TeRMIS tayari umeanza kufanya kazi katika mikoa ya Mwanza, Singida, Dodoma na Iringa ambapo kiwango cha chini cha ushughuru kwa vyombo vya moto kinaanzia shilingi 200 huku kiwango cha juu kikiwa ni shilingi laki moja vikitofautiana kulingana na aina ya chombo cha moto alichonacho.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.