LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA: MISA Tanzania yatoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) imetoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania kuhusu Sheria zinazosimamia taaluma ya habari.

Akifungua mafunzo hayo Jumamosi Agosti 28, 2021 katika ukumbi wa Hotel ya Victoria Palace jijini Mwanza, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) Andrew Marawiti amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Wahariri wa vyombo vya habari kuhusu Sheria zinazosimamia taaluma ya habari.

Marawiti amezitaja Sheria hizo kuwa ni pamoja na Sheria ya Huduma za Habari (MSA 2016), Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 na Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA 2010).

Amesema Waandishi wa Habari na Wahariri wakizifahamu vyema Sheria zinazosimamia taaluma ya Habari pamoja na Kanuni zake wataweza kutambua wajibu wao na kutimiza vyema majukumu yao huku wakizikabili changamoto zinazotokana na Sheria hizo.

Naye Afisa Programu kutoka MISA-TAN, Jacqueline Jones amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wahariri kuhusu mfumo wa Sera za Sheria za Vyombo vya Habari ili wasaidie kutumia nafasi zao kuleta mabadiliko kwa Waandishi wa Habari na Jamii kwa manufaa ya Taifa zima.

Kwa upande wake Mwezeshaji katika mafunzo hayo, Jesse Kwayu amesema Waandishi wa Habari ni kundi la watu muhimu katika kutetea masuala mbalimbali ikiwemo Sheria zinazokiuka Haki za Binadamu hivyo Waandishi wa Habari wana jukumu la kuhakikisha Haki hizo zinalindwa.

"Waandishi wa Habari ni watu muhimu katika kulinda na kutetea haki za binadamu hivyo wawe mstari wa mbele kupigia kelele Sheria zinazokiuka Haki za Binadamu na kuhakikisha hazivunjwi wala kuingiliwa" amesema Kwayu.
Na George Binagi na Kadama Malunde - Mwanza
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) Andrew Marawiti akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Waandishi wa Habari na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania kuhusu Sheria zinazosimamia taaluma ya habari.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) Andrew Marawiti akifungua mafunzo hayo.
Afisa Programu kutoka MISA-TAN, Jacqueline Jones akielezea lengo la mafunzo hayo kwa Waandishi wa Habari na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania kuhusu Sheria zinazosimamia taaluma ya habari
Mwezeshaji Jesse Kwayu akitoa mada kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu taaluma ya uandishi wa habari wakati wa mafunzo hayo.
Mwezeshaji Jesse Kwayu akitoa mada kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu taaluma ya uandishi wa habari.
Mwezeshaji Jesse Kwayu akitoa mada wakati wa mafunzo hayo.
Mwezeshaji Jesse Kwayu akitoa mada kuhusu sheria mbalimbali zinazohusu taaluma ya uandishi wa habari.
Waandishi wa Habari na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Waandishi wa Habari na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakiwa ukumbini.
Mhariri wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde akiwa ukumbini.

Picha na George Binagi na Kadama Malunde

No comments:

Powered by Blogger.