LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanahabari kuwatumia wataalamu kuondoa mkanganyiko kuhusu UVIKO 19

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wahabari nchini wametakiwa kuwatumia wataalamu wa afya katika kutoa habari zinazohusiana na UVIKO 19 na kuacha kuwapa nafasi watu wasio na taaluma ya afya kuuzungumzia ugonjwa huo ili kuondoa sintofahamu inayoendelea nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Moyo ya Jakaya Kikwete wakati wa mkutano ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Freedom House uliofanyika kwa njia ya mtandao (Zoom).

Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara hiyo, Dkt. Leornard Subi amesema hadi sasa kuna matokeo mazuri ya chanjo ya UVIKO 19 tangu ilipoanza kutolewa hapa nchini ambapo hadi sasa kuna vituo zaidi ya 1845 vinavyotoa huduma ya chanjo kote nchini na jitihada za kufika mpaka vijijini zinaendelea.

Dkt. Subi amesema Tanzania imepunguza idadi ya vifo tangu Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan alipozindua uchanjaji wa chanjo July 28 mwaka huu na kuwataka watanzania kuendelea kujitokeza katika vituo vilivyotengwa kwaajili ya kupata chanjo ili kupunguza makali ya ugonjwa huo wa UVIKO 19.

Akizungumzia umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19, Profesa Harun Nyagori ambaye ni Daktari Bingwa Mwandamizi wa magonjwa ya ndani na moyo kutoka (JKCI) amesema chanjo ya UVIKO 19 ni salama na haina madhara yoyote kwenye mifumo ya uzazi wala haisababishi kuganda kwa damu kama inavyoelezwa.

Profesa Nyagori amesema tafiti zote zilizofanywa hazionyeshi mtu atakayepatiwa chanjo ya UVIKO 19 atapata tatizo la uzazi na badala yake ilionekana kuna wanaume walipungukiwa nguvu za kiume baada kukutwa virus vya UVIKO 19 ambapo waliathirika asilimia 18 tu na baada ya kupatiwa chanjo watu hawa hurudi katika hali zao za kawaida.

Akizungumzia kuhusiana na fununu za kuganda kwa damu, Profesa Nyagori amesema kitaalamu ugonjwa wenyewe wa UVIKO 19 unaweza kusababisha kuganda kwa damu kwa mgonjwa kwa asilimia 15 lakini pia akasema kuna magonjwa mengine ambayo ni kisukari na presha husababisha damu kuganda hivyo sio sahihi kudhani kwamba chanjo inaweza kusababisha tatizo hilo.

Naye mkurugenzi wa shirika la Freedom House, Daniel Lema ameishukuru Wizara ya Afya kwa kutoa wataalamu ambao wameweza kutoa wataalamu ambao wametoa majibu ya maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa na jamii juu ya chanjo ya UVIKO 19.

Lema amewataka wataalamu kuendelewa kutoa elimu kwa jamii ili kutoruhusu uvumi wa taarifa zisizo na ukweli kupata nguvu kutoka kwa watu ambao wanalengo baya la kupotosha ukweli uliopo.

Naye Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko amewashuru wadau wote kwa kuhudhuria mkutano huo na kusema kuwa, watajitahidi kukaanda mikutano kama hiyo ili kujadili mwenendo wa chanjo ya UVIKO 19 na umuhimu wa kuchanja.
Na Tonny Alphonce, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.