LIVE STREAM ADS

Header Ads

NEMC yashusha rungu kwa makampuni ya mafuta

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt.
Samuel Gwamaka kwa mamlaka aliyopewa amevitoza faini vituo vya mafuta vinavyomilikiwa
na Makampuni mbalimbali ya uuzaji na usambazaji wa Mafuta Nchini jumla ya kiasi cha
shilingi Bilioni 5.1 kwa kushindwa kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM).
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake jijini Dar es
Salaam.
Akiongea katika Mkutano huo ametaja Kampuni zilizofungiwa pamoja na idadi ya vituo na faini
waliyotozwa kuwa ni pamoja na Oryx Tanzania L.t.d vituo kumi na tano na faini ya shilingi
milioni 750, Kampuni ya PUMA vituo ishirini na mbili na faini ya shilingi bilioni 1.1, Kampuni
ya TOTAL vituo kumi na sita na faini ya shilingi milioni 800.

Nyingine ni kampuni ya Camel vituo sita na faini ya shilingi milioni 300, Kampuni ya GBP vituo kumi na faini ya shilingi milioni 500, Kampuni ya GAPCO vituo nane na faini ya shilingi milioni 400, Kampuni ya Esta vituo tisa na faini ya shilingi milioni 450, Kampuni ya Oilcom vituo kumi na mbili na faini ya shilingi milioni 600 na Kampuni ya TSN Vituo vinne na faini ya shilingi milioni 200.

Amemaliza kwa kusema kuwa mpaka sasa Kampuni za uuzaji na usambazaji wa mafuta
zilizotozwa faini ni Kampuni 10 na tayari wameshatoza faini ya kiasi cha shilingi bilioni 3.3
Kampuni ya Lake Oil.

Mpaka sasa Kampuni zilizotozwa faini ni Kampuni kumi na NEMC bado tunaendelea na
msako kwa Makampuni yote ambayo hayajafanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na
ninawaomba wajisalimishe”.amesema Dkt. Gwamaka.
Na Rashda, Swed, Dar

No comments:

Powered by Blogger.