Bongo Star Search (BSS) 2021 Na Vipaji Viendelee
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark inayoandaa shindano la kusaka vipaji Tanzania la Bongo Star Search, Madam Lita Paulsen (katikati) akizungumzia maandalizi ya shindano hilo kwa mwaka huu 2021 baada ya kutua jijini Mwanza, Oktoba 01, 2021.
Madam Lita anasema ushindani mwaka huu utakuwa mkali kwani washiriki kutoka mikoa mbalimbali nchini wamejiandaa vyema ili kuonesha vipaji vyao ambapo amewahimiza kutumia jukwaa la BSS kutimiza ndoto zao.
Kwa Kanda ya Ziwa, usaili wa washiriki wa BSS utafanyika Oktoba 02-03, 2021 katika Hotel ya La Kairo jijini Mwanza huku Madam Lita (katikati) akiwa Jaji Mkuu ambapo atasaidiana na majaji wengine akiwemo Salama Jabir (kushoto) na Master J (kulia).
Mwaka huu 2021 Bongo Star Search (BSS) wanasema "Na Vipaji Viendelee".
No comments: