LIVE STREAM ADS

Header Ads

Musoma Vijijini wamshukuru Rais Samia kwa ujenzi wa barabara

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Na Shomari Binda, Musoma
Wananchi wa jimbo la Musoma vijijini wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

Wakizungumza kwenye mradi wa barabara mpya ya Mkirira-Kwangwa iliyofunguliwa hivi karibuni, wamesema imekuwa ni msaada mkubwa kupatikana kwa barabara hiyo.

Wananchi hao wa Kijiji cha Mkirira wamedai kipindi cha nyuma walulazimika kusafiri umbali wa kilometa 15 kwenda Hospital ya Rufaa ya Mwalimu Nyerere lakini sasa wanasafiri kwa kilometa nne.

Mmoja wa wananchi hao, Mukama Magoti amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia imekuwa na huruma kwa wananchi kwa kuwajali katika masuala mbalimbalu.

Mukama amesema licha ya barabara hiyo kuwawezesha kufika kwa haraka hospitalini lakini pia inawasaidia katika shughuli za kiuchumi.

"Tunashukuru Rais Samia kwa kuwezesha fedha na kufunguliwa kwa barabara hii na leo imetupa unafuu tofauti na miaka ya nyuma" amesema na kuongeza;

"Zipo barabara nyingine katika jimbo letu zilukuea hazipitiki lakini sasa nyingi zinapitika na tunamshukuru pia mbunge wetu, Profesa Sospeter Muhongo kwa ufuatiliaji" amesema Mukama.

Menrja wa Tarura Wilaya ya Musoma, Hussein Abbas amesema Serikali imetoa fedha zaidi ya bilioni moja wilayani humo na kazi inaendelea kwenye maeneo mbalimbalii.

Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kila eneo la jimbo kumekuwa na kasi kubwa ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na kuishukuru Serikali ya Rais Samia kwa fedha walizopata.

No comments:

Powered by Blogger.