Benki ya Exim yaunga mkono jitihada za Rais Samia kuboresha elimu
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuboresha elimu nchini, Benki ya Exim Tanzania (Exim Bank) imekabidhi madawati 100 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 ili kupunguza uhaba wa mawadati katika Shule mbalimbali za Msingi mkoani Mwanza.
Akizungumza tarehe 23 Novemba 2021 kwenye zoezi fupi la kukabidhi madawati hayo kwa uongozi wa Serikali mkoani Mwanza, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano kutoka Benki ya Exim, Stanley Kafu amesema hatua hiyo itasaidia kuboresha mazingira kwa wanafunzi kupata elimu.
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel ameipongeza benki ya Exim kwa kutimiza miaka 24 tangu kuanzishwa kwake na kuamua kurejesha fadhila kwa jamii kupitia madawati hayo kwani yatasaidia kuondoa uhitaji uliopo na kuboresha mazingira ya wanafunzi kujifunza.
“Madawati haya yataleta mageuzi makubwa kwenye mkoa wetu kwani uhitaji ni mkubwa, tuna miradi mingi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa inayoendelea baada ya kupokea fedha nyingi kutoka kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan hivyo natoa shukurani za dhati kwenu na naomba taasisi nyingine ziige mfano huu” amesema Mhandisi Gabriel.
Akipokea madawai hayo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mkuu wa Wilaya Misungwi Veronica Kessy amesema kwa kushirikiana na viongozi wenzake atahakikisha madawati hayo yanakabidhiwa katika Shule zenye uhaba na kutunzwa vyema kwa lengo la kuleta tija iliyokusudiwa hususani kukabiliana na uhaba uliopo uliotokana na mwitikio wa wazazi kupeleka watoto Shule kutokana na sera ya elimu bila ada.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (kulia) akipokea madawati 100 kutoka Mwakilishi wa Benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu (kushoto).
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (kushoto) akimkabidhi madawati 100 Mkuu wa Wilaya Misungwi Veronica Kessy (kulia). Madawati hayo yametolewa na Benki ya Exim.
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (wa nne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mkoani Mwanza na wawakilishi kutoka Benki ya Exim.
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA>>> Habari zaidi hapa
No comments: