LIVE STREAM ADS

Header Ads

MPC na Freedom House zawashukuru wataalamu wa Afya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com 
Klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC) na Shirika la Kimataifa la Freedom House wamewashukuru wataalamu wa afya toka Wizara ya Afya,  ustawi wa jamii, Wazee  jinsia na watoto kwa kushiriki kikamifu kwenye majadiano ya mtandaoni ya waandishi wa habari na Asasi Zisizo  za Kiserikali(AZAKI).

Alex Mchomvu, Makamu Mwenyekiti wa MPC wakati wa hotuba yake ya ufunguzi alisema kuwa, anawashukuru sana wataalamu ambao ni madaktari kwa kujitoa kwao kwa ajili ya kushiriki majadiliano ya waandishi wa habari na AZAKI.

Kwa upande wa Mwakilishi toka Freedom House Afisa Programu  Lina Muro  alisema kuwa, anaishukuru sana Wizara kwa kutoa wataalamu ambao wamekuwa wakitumika kutoa elimu kwenye maadiliano hayo ya kila mwezi.

Pia Lina  aliwashukuru washiriki wote kwa kujitokeza na kuhudhuria majadiliano hayo ya Mwezi Oktoba, 2021.

Mchomvu aliongeza kuwa, majadiliano hayo ya kila mwezi yenye kulenga kujua maendeleo ya chango ya UVIKO 19 yana umuhimu mkubwa kwa kuwa kundi la waandishi wa habari linahitaji elimu zaidi ya chanjo ya UVIKO 19 ili jamii ipate taarifa sahihi.

Hivyo kuwepo kwa wataalamu kunasaidia kuondoa uzushi wa habari za uongo juu ya chanjo ya UVIKO 19.

Wataalamu hao Profesa Haroun Ngonyani toka Hospitali ya Jakaya Mrisho Kikwete na Daktari Baraka Nzobo toka Hospitali ya Muhimbi walishiriki majadiliano haya ya mtandaoni na kutoa elimu juu ya mwenendo wa chanjo ya UVIKO 19.

Kwa upande wake wake Profesa Ngonyani alisema kuwa, kwa kiasi kikubwa watanzania wamejitokeza kwa uwingi kwenye zoezi la kupata chanjo tofauti na awali kabla ya kuanza kampeni ya chanjo ya UVIKO  19.

Pia alisema kuwa, maeneo ya Vijijini yameonyesha kuwa na mwamko mkubwa wa watu kujitokeza kuchanja kuliko Mijini.

Majadiliano hayo yaliandaliwa kwa pamoja kati ya Klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza na Taasisi ya Freedom House na kuhudhiriwa na washiriki zaidi ya tisini.
Na Mwandishi Maalum, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.