LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yaridhia Jumeme kupandisha bei ya umeme

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Nishati, January Makamba amesema bei mpya ya nishati ya jua inatarajiwa kuongezeka kutoka shilingi 100 kwa tokeni moja hadi shilingi 1,600 lengo likiwa ni kuwezesha upatikanaji wa uhakika na kuondoa adha kwa wananchi. 

Waziri Makamba ameyasema hayo Januari 12, 2022 alipofanya ziara ya kukagua miundombinu ya nishati ya jua katika Kisiwa cha Ukara Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza inayoendeshwa na kampuni ya Jumeme. 

Gharama hizo zilishushwa na Serikali miaka miwili iliyopita kutoka shilingi 3,500 kwa tokeni moja hadi shilingi 100 hatua ambayo iliilazimu kampuni ya Jumeme kupunguza uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme katika maeneo ambayo hayajafikiwa na mtandao wa nishati ya TANESCO.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.