LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wizara ya Ardhi yaweka wazi Utekelezaji wa Vipaumbele vyake

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MUHTASARI WA VIPAUMBELE KATIKA UTEKELEZAJI WA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23 13 JULAI, 2022 MWANZA

MUHTASARI WA VIPAUMBELE KATIKA UTEKELEZAJI WA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23 1.0 UTANGULIZI 
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inahusisha idara kuu za kisekta ambazo ni: Utawala na Maendeleo ya Ardhi, Upimaji na Ramani, Maendeleo ya Makazi na Uthamini. 

Vitengo vikuu vya sekta ni Usajili wa Hatimiliki, Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya na Uendelezaji Miliki. Mbali na hayo, Wizara ina Idara na Vitengo mbalimbali vinavyosaidia kuongeza ufanisi wa kazi katika wizara kama vile Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Fedha na Hesabu, Ukaguzi wa Ndani, Huduma za Sheria, Sera na Mipango, Mawasiliano na Teknolojia (TEHAMA), Mawasiliano Serikalini na Usimamizi wa Manunuzi. 

Kadhalika ofisi za Utawala wa Ardhi katika Mikoa 26. Kadhalika Wizara ina tume inayoshughulikia Mipango ya Matumizi ya Ardhi na pia Shirika la Nyumba la Taifa. Kimsingi majukumu ya wizara yanalenga kuwezesha usimamizi madhubuti wa ardhi na huduma za maendeleo ya makazi ya watu kwa ajili ya kuboresha ustawi wa kijamii na kiuchumi - kwa jamii ya Kitanzania.

 1.1 MAJUKUMU YA WIZARA 
Kwa mujibu wa Tangazo la Serikali (GN Na. 385) la tarehe 7 Mei, 2021; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ina majukumu yafuatayo: 

i. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995; 
ii. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Makazi ya mwaka 2000; 
iii. Kusimamia utawala wa ardhi; 
iv. Kusimamia upangaji na uendelezaji wa miji na vijiji; 
v. Kusimamia na kuwezesha upimaji wa ardhi na kutayarisha ramani; 
vi. Kumilikisha ardhi na kuwezesha utoaji wa hati za hakimiliki ya kimila; 
vii. Kusajili hatimiliki za ardhi, miamala na nyaraka za kisheria; 
viii. Kusimamia uthamini wa mali nchini; 
ix. Kuhamasisha na kuwezesha ujenzi wa nyumba bora; 
x. Kusimamia uendelezaji milki; 
xi. Kusimamia utunzaji wa kumbukumbu za ardhi; 
xii. Kusimamia ukusanyaji wa maduhuli yatokanayo na huduma za Sekta ya Ardhi; 
xiii. Kuwezesha uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi na kufuatilia utekelezaji wake; 
xiv. Kusimamia taasisi zilizo chini ya Wizara ambazo ni Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi; Shirika la Nyumba la Taifa na Vyuo vya Ardhi vya Tabora na Morogoro; na 
xv. Kusimamia maslahi, utendaji kazi na maendeleo ya watumishi wa Wizara. 

2.0 VIPAUMBELE KATIKA MPANGO WA UTEKELEZAJI WA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23 
Katika mwaka 2022/23, Wizara inatarajia kukusanya shilingi bilioni 250.1 kutokana na maduhuli ya Sekta ya Ardhi kwa kutekeleza mikakati ambayo imeainishwa katika Hotuba ya Bajeti. Hivyo katika mwaka wa fedha 2022/23 Wizara imejipanga kuhakikisha inatekeleza yafuatayo: 

2.1 Kuimarisha Matumizi ya TEHAMA 
✓ Wizara itaendelea kujenga, kusimika na kuimarisha miundombinu wezeshi ya TEHAMA kwa awamu katika Ofisi za Ardhi za Mikoa na Halmashauri nchini. 
✓ Vilevile, ukarabati wa mtandao kiambo katika Ofisi za Halmashauri 47 zikiwemo Makao Makuu ya Mikoa ya Iringa, Lindi, Mwanza na Mbeya utafanyika; 
✓ kukamilisha kazi ya kubadilisha Michoro ya Mipangomiji, Ramani za upimaji Ardhi, Nyaraka za umiliki zilizobaki kutoka analojia kwenda digitali. 

2.2 Usalama wa Miliki za Ardhi 
✓ Kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Milki za Ardhi (Land Tenure Improvement Project) – LTIP 
▪ Mradi huu utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano (2022/23 – 2027/28) 
▪ Kupitia mkopo wa riba nafuu USD milioni 150, 
▪ Mradi utajenga Ofisi za Ardhi katika Mikoa 25 zitakazokidhi utoaji huduma kwa Mfumo Unganishi wa Kuhifadhi Taarifa za Ardhi (ILMIS). Pia, huduma zote za sekta zitakuwa zikitolewa katika majengo hayo zikiwemo huduma za Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya.

✓ Katika mwaka 2022/23 kipaumbele ni: 
▪ Kujenga ofisi za Ardhi za mikoa: ▪ Kuboresha mfumo wa ILMIS; 
▪ Kutoa Hatimiliki 150,000 katika Halmashauri 10; 
▪ Kutoa Hati za Hakimiliki za Kimila 50,000 katika Vijiji 50; 
▪ Kuandaa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji 50 katika Wilaya sita (6) na Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Wilaya hizo; 
▪ Kutoa Leseni za Makazi 250,000. 

2.3 Kuimarisha Miundombinu ya Upimaji na Ramani 
✓ Kupitia Mradi wa Uimarishaji wa Miundombinu ya Upimaji na Ramani – NSDI. 
▪ jumla ya fedha za mkopo wa riba nafuu wa USD milioni 65 kupitia Benki ya Exim. 
▪ Manufaa ya mradi huu ni utawezesha kuongeza kasi ya upangaji na upimaji ardhi, uwezo wa kuandaa ramani za msingi kwa nchi nzima ambazo zinahitajika kwa matumizi mengine hususan ya ujenzi wa miundombinu msingi ya umma. 

2.4 Upangaji Miji na Maendeleo ya Makazi 
✓ Katika kulinda maeneo yanayochipukia kuwa miji, 
▪ Wizara imekwisha andaa mwongozo wa kusimamia uandaaji wa mipango ya uendelezaji wa makazi na ujenzi wa nyumba vijiji ambao unaelekeza namna ya kupanga makazi vjijini kwa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa. 

▪ Wizara inandaa mafunzo kwa wananchi kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa upangaji na usimamizi kwa miji midogo katika maeneo ya vijiji. 

2.5 Urasimishaji Makazi 
✓ kwa kushirikiana na Mamlaka za Upangaji na sekta binafsi ikiwa ni hatua ya kukamilisha Programu ya Kurasimisha Makazi na Kuzuia Makazi Yasiyopangwa Mijini (2013 - 2023). Baada ya muda uliopangwa kutekeleza programu ya urasimishaji kuisha, Wizara itafanya tathmini ya mafanikio na changamoto ya utekelezaji wa programu hii.
✓ Inaendelea kusisitiza wananchi wote wanaoishi katika maeneo ambayo hayajapangwa kuendelea kushiriki kikamilifu katika zoezi la urasimishaji ikiwemo kuchangia gharama za urasimishaji na gharama za hati ili waweze kurasimishiwa maeneo yao na kupata haki miliki za viwanja vyao. 

2.6 Migogoro ya Ardhi Wizara imejipanga kuhakikisha inatatua na kudhibiti migogoro ya ardhi kwa kutumia njia mbalimbali na kuhusisha Wizara za kisekta na wadau wa Sekta ya Ardhi. Njia hizo ni pamoja na: 
✓ kubadilisha nyaraka za upangaji, upimaji na umilikishaji ardhi kutoka analogia kuwa za kidigitali kama mpango wa muda mrefu katika kupunguza migogoro; 
✓ kutoa elimu kwa umma kwa kushirikiana na wadau mbalimbali; 
✓ kuongeza kasi ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi; 
✓ madawati ya kushughulikia malalamiko katika Ofisi za Ardhi za Mikoa; na 
✓ kuwepo Rejista ya migogoro ya ardhi kwa kila Ofisi za Ardhi za Mikoa na Halmashauri. Rejista hizo zinayoonesha aina na hali ya mgogoro pamoja na namna ulivyoshughulikiwa. 

2.7 Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya 
✓ kuwezesha Mabaraza mapya 59 kuanza kutoa huduma na hivyo kuwa na Mabaraza yanayotoa huduma katika Wilaya zote nchini. 
✓ kukamilisha ujenzi wa Mfumo wa Kusimamia Mashauri katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya (Intergrated Land Cases Management System) na kuanza kutumika. Lengo ni kurahisisha utendaji kazi wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya katika: 
▪ kutunza kumbukumbu za mashauri; 
▪ kufungua mashauri mapya; 
▪ kufuatilia utendaji kazi wa watumishi wa Mabaraza; na 
▪ upatikanaji wa nakala za hukumu kwa njia ya mtandao.  

2.8 Utawala Bora na Uwajibikaji 
✓ Wizara inatambua umuhimu wa kuimarisha mifumo ya utawala bora, uwajibikaji na kudhibiti ukiukwaji wa maadili kwa watumishi wa sekta ya Ardhi. Katika mwaka 2022/23, Wizara inaanzisha Mfumo wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi (Land Governance Framework) ambao utaongeza uwajibikaji, uwazi na ufanisi katika kutoa huduma za sekta. 

2.9 TUME YA TAIFA YA MIPANGO YA ARDHI 
Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya ardhi inatekeleza makumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Upangaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya mwaka 2007, maelekezo na miongozo ya Serikali katika kufikia malengo makubwa ya Serikali yaliyoanishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo (TDV 2025) ambayo hutekelezwa kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Mpango wa tatu wa Taifa wa miaka 5 (2021/22-2025/26) ambao umebeba vipaumbele vya Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.

 Jukumu kubwa la Tume ni kuwezesha, kuratibu na kusimamia Mamlaka za upangaji katika kuhakikisha inaandaa mipango ya matumizi ya ardhi nchini na kuitekeleza. Jukumu hili hufanywa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo Halmshauri zetu. 

Katika mwaka wa fedha 2022/23 vipaumbele vya Tume kufanya yafuatayo: 
✓ Kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya Wilaya 2 katika maeneo yaliyopitiwa na miradi ya Kimkakati; 
✓ Kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya Vijiji 170 kwa fedha ya Serikali na vijiji 120 kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa mwaka katika maeneo yenye miradi ya kimkakati ifuatayayo: 
▪ ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), 
▪ Mradi wa ufuaji wa umeme wa Bwawa la Julius Nyerere, 
▪ Mradi wa Mkuza wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki (EACOP); na 
▪ vijiji vinavyopakana na nchi Jirani na vyenye migogoro ya ardhi 

✓ Kuandaa mipango kina 20 itakayowezesha wananchi upangaji, upimaji na umiliki wa ardhi kwa wananchi;  
✓ Kufanya Ukaguzi wa uzingativu wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi iliyoandaliwa katika vijiji 50 kwenye miradi ya kimkakati; 
✓ kuboresha mfumo wa utunzaji wa kumbukumbu wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi; 
✓ Kufanya ufuatiliaji na Tathimini katika vijiji 50 vilivyoandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi; 
✓ Kutoa elimu na kuzijengea uwezo mamlaka za upangaji 30 katika kuandaa, kulekeleza na kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi 

2.10 SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA 
Majukumu ya Shirika yanatekelezwa kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Shirika wa Miaka 10 (2015/16 – 2024/25) ambao unalenga: 
✓ kukamilisha miradi ya Shirika iliyo katika hatua mbalimbali; ✓ kufanya ukarabati wa majengo ya shirika; 
✓ kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya uzalishaji wa vifaa vya ujenzi; 
✓ kujenga majengo ya biashara na nyumba za gharama nafuu katika maeneo mbalimbali; 
✓ kuendeleza Miji ya Pembezoni (Satellite Towns); na 
✓ kutekeleza miradi mbalimbali ya ukandarasi. 

Katika mwaka wa fedha 2022/23 Shirika limepanga kufanya yafuatayo: 
✓ Kukusanya shilingi bilioni 268.03 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato; 
✓ Kuendelea na ujenzi wa mradi wa nyumba 1,000 za gharama nafuu Jijini Dodoma kwa ajili ya kuuza na kupangisha; 

✓ Kukamilisha ujenzi wa Mradi wa Morocco square na kuendelea na Miradi katika Kiwanja Na. 711 Kawe, Golden Premier (GPR-Project) na ujenzi wa nyumba 500 katika eneo la Kawe kwa ajili ya wananchi wa kipato cha kati cha chini ambapo nyumba 360 zitajengwa awamu ya kwanza na nyumba 140 zitajengwa awamu ya pili; 

✓ Kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa michoro katika miji ya pembezoni (Satellite Cities) ya Kwala – Ruvu, Mbezi One Riffle Range (Dar es Salaam) na Kawe; 
✓ Kuendelea na ujenzi wa majengo ya biashara katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Bukoba, Mwanza, Dodoma, Kahama, Morogoro, Masasi na Lindi; 

✓ Kuandaa Mpango Kabambe wa matumizi ya ardhi katika maeneo ya Iwambi na Mwashiwawala – Mbeya, Uvumba – Dar es Salaam na Mafuru Village - Morogoro;  

✓ Kuendelea na utekelezaji wa miradi ya ukandarasi ikiwemo ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Wizara nane (8) Jijini Dodoma, ujenzi wa Jengo la Shule ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ujenzi wa majengo matano (5) ya Wakala wa Ununuzi wa Serikali (GPSA), ujenzi wa jengo la TANZANITE Mirerani, ujenzi wa Jengo la Kitengo cha Moyo cha Jakaya Kikwete (JKCI) na miradi mingine itakayojitokeza; 

✓ Kuendelea na usimamizi wa miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo Soko la Kariakoo; 
✓ Kuendelea kutekeleza Mpango wa miaka mitano wa ukarabati wa nyumba za Shirika unaoishia mwaka 2027; 
✓ Kununua ardhi ekari 400 katika maeneo mbalimbali ya kimkakati kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na akiba ya ardhi; 

✓ Kuanza utekelezaji wa Sera ya Ubia itakayoruhusu Sekta Binafsi kushiriki katika uendelezaji wa maeneo ya Shirika; 
✓ Kuendelea na ujenzi wa viwanda vya kuzalisha vifaa vya ujenzi hususan kokoto na matofali; 
✓ Kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya nyumba na kulitangaza Shirika na Sekta ya Milki nchini kupitia vyombo vya Habari na; 

✓ Kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuandaa eneo na baadae kujenga Sports Arena itakayochochea ukuaji wa mji wa kitovu cha mji wa Kawe.
Tazama BMG TV LIVE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.