LIVE STREAM ADS

Header Ads

Dodoma: DC Mwema awataka wahitimu JKT kuzingatia uzalendo kwa Taifa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remidius Mwema amesema Taifa lolote lenye vijana imara wenye kuendelea kusimamia misingi ya nchi na kufanya kazi kwa bidii Taifa hilo litayafikia maendeleo yake kwa haraka na endapo tu kila mmoja ataweka uzalendo mbele.

Kauli hiyo ameitoa wakati akifunga mafunzo ya vijana wa mujibu wa Sheria yaliyofanyika wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Alisema ana matumaini makubwa na vijana wa mujibu wa Sheria waliomaliza mafunzo hayo wamejifunza mambo mengi ya msingi walipokuwa mafunzoni na hilo limejidhihirisha kupitia gwaride na maonyesho ya vikundi mbalimbali.

“Mlipokuwa hapa mmejifunza uzalendo kwa kuunganishwa na vijana wengine kutoka maeneo mbalimbali ya nchi yetu, ili muweze kudumisha upendo, umoja na mshikamano miongoni mwenu na kulipenda Taifa lenu na kufanya kazi bila kubaguana” alisema Mwema

Aliwataka vijana hao kudumisha uzalendo, ukakamavu pamoja na kufanya kazi na kulitumikia Taifa lao pendwa la Tanzania.
“Mmejifunza mafunzo ya awali ya kijeshi kwa nadharia na vitendo, jambo ambalo limewajengea ujasiri, ukakamavu na utayari wa kutetea Taifa dhidi ya maadui wa ndani na WA nje hivyo kuwa sehemu ya Jeshi la akiba la JWTZ, tambueni kwamba Kupitia mafunzo haya ninyi mmekuwa askari wa akiba wa Taifa letu basi mtakapohitajika muwe tayari kulitumikia Taifa” aliongeza.

Aidha alisema kila mmoja anafahamu umuhimu wa uzalendo kwa nchi hivyo ni matumaini yake kwamba mafunzo ya uzalendo waliyoyapata yataleta mafanikio kwa Taifa na hasa vijana ambao ni Taifa la leo kwa nchi.

Katika taarifa yao wahitimu hao walimweleza mgeni rasmi wakiwa mafunzoni hapo walijifunza masomo mbalimbali kama vile utimamu wa mwili, mafunzo mbalimbali ya kijeshi, historia ya JKT pamoja na uraia.

“Ndugu mgeni rasmi mafunzo haya yametufanya kuwa watii, hodari, waaminifu pia kuweza kuwa na moyo wa kujitolea kukabiliana na kupambania na majanga yote ambayo yanaweza kutokea Katika Taifa letu." ilisema sehemu ya risala hiyo.

Katika risala hiyo wahitimu hao kupitia Operesheni Jenerali Venance Mabeyo kikosi cha 826 KJ Mpwapwa walizungumzia changamoto mbalimbali ikiwemo udogo wa eneo la kikosi kwani lilisababisha baadhi ya shughuli kushindwa kufanyika ndani ya kikosi na kupelekea kufanyika nje ya kikosi.
Changamoto ya pili ni tatizo la mtandao, kwani ililazimika baadhi ya vijana kwenda mjini kwa ajili ya kufanya udahili wa vyuo na Kupitia changamoto hiyo baadhi ya vijana walikuwa wakikosa vipindi ipasavyo.

Akijibu changamoto hizogeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Remidius Mwema aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya Mpwapwa alikiri kuzipokea na kuahidi kuwasiliana na mamlaka husika ili zipatiwe ufumbuzi.

Akitoa taarifa ya mafunzo hayo Mwakilishi wa Mkuu wa JKT Col. George Kazaula alisema vijana hao wamejifunza masomo mbalimbali ya stadi za Maisha, pamoja na mazoezi ya kijeshi na wamekuwa ni vijana wenye utimamu, lakini pia wamejifunza ujasiliamali, kilimo cha bustani na utunzaji wa mifugo.

Aidha aliwasihi vijana hao wahitimu wakaendeleze umoja, uzalendo, wakawe na nidhamu kwa viongozi wao, walimu na kuwa msaada kwa wazazi wao na watanzania kwa ujumla .

No comments:

Powered by Blogger.