LIVE STREAM ADS

Header Ads

Hali ya usalama wa watoto na kushamiri kwa vitendo vya ukatili dhidi yao

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Picha:VietNam News
“Wazazi na walezi tuwekaribu na watoto wetu, tujue changamoto wanazopitia na tutege muda kwa ajili ya watoto ili hata kama anafanywa kitu kibaya ina kuwa rahisi kumuelezea mzazi” Bi Peris Lumambo ni afisa Ustawi wa jamii wilaya ya Mvomero

Na SELEMAN E. MAHINYA
Siku za hivi karibuni, ripoti na taarifa kuhusu kushamiri kwa matukio ya vitendo ukatili wa kijinsia vimekuwa vikishamiri kwa kiasi kikubwa na vikigusa makundi mbalimbali ya jamii kuanzia wanawake, wanaume na hata kundi la watoto ambalo linaonekana kuwa muhanga mkubwa kwa siku za hivi karibuni.

Ukatili wa kijinsi kwa watoto wadogo unahusisha vitendo vya ubakaji,ulawiti na ndoa za utotoni, na vitendo hivi vya kikatili kwa kiasi kikubwa vinatajwa kufanywa na watu wa karibu katika familia na jamii . hivi karibuni mkoani mwanza mtoto wa miaka 12 ‘Huruma’ (si jina halisi) aliripotiwa kulawitiwa na moja wa jirani yao mwanaume mwenye umri wa miaka 50. Mama mzazi anadai kuwa mtoto huyo alitoeka kwenye mazingira ya kutetanisha baada ya ubishani na ndugu yake ya juu nani aoshe vyombo.

“Alirudi saa sita kasoro usiku ,alivyorudia alirudi na wasiwasi sana tukaja kumuangalia mtoto kageuza nguo ya juu na traki alivyo vaa chini kageuza nyuma mbele mbele nyuma,jezi kagezi na yenyewe nje ndani,ndani nje na ikiwa imechanika” alisema mzazi wa mtoto huyo aliyefanyiwa ukatili huo.

“Mtoto alipohojiwa akafunguka, alipofunguka tukampigia mwenyekiti wa mtaa akaja alipokuja kutawa tumekaa kikao mwenyekiti na huyo jirani na sisi kama familia ambao ni wazazi mwenyekiti akato ushauri yakwamba twende polisi na usiende kwa mtuhumiwa wala tusimuulize tukakubali ushauri wake’’ Aliongeza mama wa mtoto muhanga wa kutio hilo la kikatili.

Mama mzazi wa ‘Huruma’ akielezea tukio la ukatili wa kijinsia alilofanyiwa mtoto wake na jirani yake mwenye umri wa 50.

Ukatili aliyofanyiwa mtoto ‘Huruma’ ni moja kati ya matukio zaidi ya elfu moja yanayotokea nchi na kuathiri maisha ya maelfu ya watoto. Lakini swali la msingi hapa ni Je, nini ninapelekea kushamiri kwa vitendo hivi katika jamii yetu ya watanzania.

Baadhi ya Sababu kama imani za potofu za kishirikina, utandawazi, malezi yasiyo bora kwa watoto na kuporomoka kwa maadili kwa jamii na matatizo ya afya ya akili kumechagia kwa kiasi kikubwa kushamiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto hapa nchini.
Mchoro ukionesha takwimu za matukio ya ukatili wa kijinsia kwa watoto nchini kwa mwaka 2021.

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la linalojishughulisha na kukomesha ukatili dhidi ya watoto na vijana ,hasa ukatili dhidi ya wasichana lijulikanalo kama Together for girls linataja mazingira ambayo ni nyumbani,mashuleni,mashirika ya dini,mitandaoni na kadhalika
Mchoro ukionesha mazingira mbalimbali ambayo ukatili wa kijinsia kwa watoto unaripotiwa, uhusiano baina ya mtoto na watu wanaowafanyia ukatili wa aina hiyo katika jamii ,muktadha wa matukio na aina ya ukatili. Kwa mujibu wa shirika la Together for girls 2021.
Mwenyekiti Mwenza wa Jukwaa la Amani Gairo Mchungaji Canon Benedict Mbelwa.
 (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo:GAIRO)

“Lazima sisi viongozi wa dini tuongee na waumini wetu na kuwaleza ukweli kuhusu ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea. Bila kusema ukweli ukatili utaendelea kuongezeka”. Alisema Mchungaji Canon Mbelwa.

Canon Mbelwa ambaye ni Mwenyekiti Mwanza wa Jukwaa la Amani Gairo alisema endapo jamii haitaelezwa ukweli kuhusu athari za matendo ya ukatili huo, kundi linalo athirika zaidi ni kundi la watoto hali inayoweza kuwaathirika kisaikolojia na kuporomosha maendeleo yao kitaaluma.

“Tusipo sema ukweli kwa waumini wetu kuhusu hili tatizo, watakaoathirika zaidi ni watoto, wanapoona matukio ya aina hii yakifanywa na wazazi wao, yanawatoa kwenye mfumo bora wa maisha, wanaharibika kisaikolojia, napengine vitendo vya ukatili vikachochea kushusha uwezo wao kitaaluma mashuleni”. Alifafanua Mchungaji Mbelwa.

Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Nuhu Jabir Mruma anasema ili kuondokana na hali hii, viongozi wa dini wachunge maadili yanayotokana na mafundisho ya vitabu vitukufu, na akieleza kuwa jamii kubwa imeacha mafundisho.

“Jamii ikichukua mafundisho na maamrisho yao tutaondoka huko, pia viongozi wa dini wawe mifano katika yale wanayohubiri katika makanisa na misikiti, tumesikia mengi yanayozungumzwa yaliyofanyika, huenda ni kweli au si kweli ila wawe mifano.

“Lakini wazazi pia wafuatilie miendeno na maendeleo ya watoto wao na tabia zao shuleni, pia wajue mienendo na misimamo ya shule wanazopeleka watoto wao ili kuhakikisha wako salama,” alisema Mruma.

Kwa upande serikali kupitia kwa waziri wa wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia wanawake watoto na watu wenye mahitaji maalumu wanakiri ya kwamba kasi ya kupungua ukatili kwa watoto ni ndogo hapa nchini.

“Mwaka 2020 -2021 kupungua wa asiliamia 27 tu ,lazima twende kutaifuel ili ipungue kwa haraka ,tunafanyaje ndiyo mtihani uliyopo kwa sasa”

alisema waziri dorothy Gwajima wakati wa kufungua washa ya kuzungumza uingwazwaji wa masuala ya ulinzi na afya ya uzazi kwa vijana na wanawake kuingizwa katika rasimu ya katiba mpya jijini Dar es salaam.

“Uliotarajiwa ifikapo mwaka 2022 kutoka mwaka 2017-2018 iwe imepungua kwa asilimia 50 lakini mbona tunakwenda nkwa kasi ndogo,tuanzisha kampeni huru kwa jamii,jamii ya wapenda haki,watu wenye hofu ya mungu,watu wanaokerwa na mambo ya ukatili ,watu ambao ni watetezi wa watoto,watetezi wa masuala ya kijinsia ,kampeni hii imekwenda kwa jina la Shujaa wa Maendeleo na ustawi wa Jamii Tanzania SMAUJATA” Aliongeza waziri Gwajima.
Waziri Dkt. Gwajima akizungumzia kampeni ya SMAUJATA ya kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto.

Ustawi wa jamii ni miongoni mwa wadau muhimu katika kupambana na kutokomeza ukatili wa kijinsi kwa watoto,Bi Peris Lumambo ni afisa Ustawi wa jamii wilaya ya Mvomero yeye amewataka wadau mbalimbali wakiwemo wazazi na walezi kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika malezi ya watoto wao.

“Katika suala zima la malezi watoto wanafanyiwa ukatili na ndugu zao wa karibu,kwa mfano mtoto analala na mjomba wake wakati mwingine baba yake kwahiyo unakuta mtoto anabakwa wakati mwingine kulawitiwa, kwahiyo hali ni mbaya kwahiyo wito wangu kama wanajamii, wazazi na walezi tuwekaribu na watoto wetu tujue ,tujue changamoto wanazopitia na tutege muda kwa ajili ya watoto ili hata kama anafanywa kitu kibaya ina kuwa rahisi kumuelezea mzazi” alisema Bi Peris.
Afisa Ustawi wa Jamii akielezea umuhimu wa malezi katika kukomesha ukatili wa kijinsia kwa watoto.

No comments:

Powered by Blogger.