Utoaji chakula kwa wanafunzi waleta tija Shule ya Msingi Butimba B, Mwanza. CPB yaunga mkono mpango huo
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Shule ya Msingi Butimba B iliyopo jijini Mwanza imeendelea kushirikiana vyema na wazazi pamoja na wadau mbalimbali ili kufanikisha mpango wa utoaji uji na chakula cha mchana kwa wanafunzi wote wa shule hiyo.
Akizungumza Machi 25, 2023 wakati wa zoezi la kupokea mchele tani moja kutoka Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Kanda ya Ziwa, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Josephat John amesema awali mpango huo wa hiari ulianza kwa kuwashirikisha wanafunzi takribani 300 ambao wazazi wao waliridhia kuchangia chakula.
Amesema baada ya kubaini kwamba mpango huo umesaidia kuondoa utoro wa watoto na kuinua kiwango cha ufaulu, Shule hiyo kupitia Kamati ya Chakula imeanzisha mkakati wa kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kusaidia upatikanaji wa chakula na uji kwa wanafunzi wote zaidi ya 600 shuleni hapo.
Mwl. John ameishukuru Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Kanda ya Ziwa ambayo imeunga mkono mpango huo kwa kutoa tani moja ya mchele na kuwahimiza wadau wengine kwa kushirikiana na wazazi kuendelea kuchangia upatikanaji wa uji na chakula cha mchana kwa ajili ya wanafunzi kwani hatua hiyo inaimarisha uwezo wa wanafunzi kujifunza.
Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mwl. Mussa Lambwe ametumia fursa hiyo kuwahimiza wazazi kuchangia upatikanaji wa uji na chakula kwa ajili ya wanafunzi na kuondoa dhana kwamba elimu ni bure kwani si kweli bali kuna elimu bila ada huku pia akiwataka Waratibu Elimu Kata kuweka juhudi ili kuhakikisha Shule wanazosimamia zinatoa huduma hiyo kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Kaimu Meneja Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (TCB) Kanda ya Ziwa, Alfred Kalimenze amesema taasisi hiyo kupitia kiwanda chake kilichopo Butimba imekuwa ikichakata tani 96 za nafaka na mazao mbalimbali kwa siku na kwamba matarajio ni kusimika mitambo mingine kwa ajili ya uzalishaji wa ungalishe yenye uwezo wa kuchakata tani 125 hivyo itaendelea kushirikiana na jamii ikiwemo kuboresha upatikanaji wa elimu bora ili kuunga mkono jitihada za Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Butimba B, Neema Alphonce amesema utoaji uji asubuhi na chakula cha mchana kwa wanafunzi kunawawezesha kuzingatia vipindi vya darasani na kuchochea kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.
Jitihada hizo za Shule ya Msingi Butimba B zimesaidia Shule hiyo kuongeza wigo wa ufaulu kwa miaka ya hivi karibuni na kuibuka na tuzo mbalimbali ambapo matokeo ya darasa la saba kitaifa mwaka 2020 ilikuwa ya tatu, mwaka 2021 nafasi ya nne na mwaka 2022 nafasi ya tatu kwa ufaulu wa daraja A na B pekee.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wawakilishi mbalimbali wakiwa kwenye mapokezi ya mchele tani moja kutoka Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Kanda ya Ziwa kwa ajili ya mlo wa mchana kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Butimba B iliyopo jijini Mwanza.
Wawakilishi mbalimbali wakiwa kwenye mapokezi ya mchele tani moja kutoka Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Kanda ya Ziwa kwa ajili ya mlo wa mchana kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Butimba B iliyopo jijini Mwanza.
Wawakilishi mbalimbali wakiwa kwenye mapokezi hayo.
Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mwl. Mussa Lambwe akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi mchele tani moja kwa Shule ya Msingi Butimba B jijini Mwanza uliotolewa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Kanda ya Ziwa.
Afisa Elimu Kata ya Butumba jijini Mwanza, Mwl Cecilia Tegile akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi mchele tani moja kwa Shule ya Msingi Butimba B jijini Mwanza uliotolewa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Kanda ya Ziwa.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Butimba B, Mwl. Josephat John akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi mchele tani moja kwa Shule ya Msingi Butimba B jijini Mwanza uliotolewa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Kanda ya Ziwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Butimba B jijini Mwanza, Brudele Dokta akitoa salamu zake wakati wa zoezi la kukabidhi mchele tani moja kwa Shule ya Msingi Butimba B jijini Mwanza uliotolewa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Kanda ya Ziwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Chakula Shule ya Msingi Butimba B jijini Mwanza, Kabuga Bejumula akitoa shukurani kwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Kanda ya Ziwa kwa kutoa msaada wa mchele tani moja katika Shule hiyo ili kuwezesha wanafunzi kupata mlo wa mchana wakiwa shuleni.
Kaimu Meneja Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Kanda ya Ziwa, Alfred Kalimenze akieleza namna taasisi hiyo ilivyoguswa na jitihada za uongozi wa Shule ya Msingi Butimba B na kuwaunga mkono kwa kutoa mchele tani moja ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mlo wa mchana.
Wawakilishi mbalimbali wakiwemo waalimu, wanafunzi na viongozi wa Halmashauri na Serikali ngazi ya Kata wakimsikiliza Kaimu Meneja Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Kanda ya Ziwa, Alfred Kalimenze.
Afisa Masoko Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Kanda ya Ziwa, Ally Mango akitoa salamu wakati wa makabidhiano hayo.
Mmoja wa wanafunzi Shule ya Msingi Butimba B, Neema Alphonce akitoa shukurani kwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) baada ya kutoa msaada wa mchele tani moja kwa ajili ya chakula cha wanafunzi shuleni hapo.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mapokezi ya mchele tani moja kutoka Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Kanda ya Ziwa.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Butimba B, Mwl. Josephat John akieleza namna utoaji uji na chakula kwa wanafunzi ulivyosaidia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa Shule hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Butimba B, Mwl. Josephat John akionesha tuzo mbalimbali ambazo Shule hiyo ilitunukiwa baada ya kufanya vizuri katika ufaulu.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Butimba B, Mwl. Josephat John akionesha tuzo mbalimbali ambazo Shule hiyo ilitunukiwa baada ya kufanya vizuri katika ufaulu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Butimba B jijini Mwanza, Brudele Dokta akipokea mchele kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wa Shule hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Chakula Shule ya Msingi Butimba B jijini Mwanza, Kabuga Bejumula (kulia) akishiriki mapokezi ya mchele kutoka CPB.
Afisa Elimu Kata ya Butumba jijini Mwanza, Mwl Cecilia Tegile (kushoto) akishiriki zoezi la kupokea mchele uliotolewa na CPB kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wa Shule ya Msingi Butimba B.
Baadhi ya waalimu Shule ya Msingi Butimba B wakipokea mchele.
Viongozi mbalimbali Kata ya Butimba wakipokea mchele kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wa Shule ya Msingi Butimba B jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali Kata ya Butimba wakipokea mchele kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wa Shule ya Msingi Butimba B jijini Mwanza.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mapokezi hayo.
SOMA>>> Habari zaidi hapa
No comments: