LIVE STREAM ADS

Header Ads

TACAIDS yawasilisha taarifa kuhusu miundo na majukumu yake kwa kamati ya Bunge ya Afya na UKIMWI

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu, Mhe George Simbachawene  akizungumza na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI walipokutana na TACAIDS wakati wa wasilisho la muundo na majukumu ya TACAIDS kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI katika Ukumbi wa Ofisi za Bunge jijini Dodoma, Leo Machi,12, 2023.

Na Nadhifa Omar, Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe.George Simbachawene amesema Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kutoa ushirikiano unaostahiki kwa kamati ya Afya na masuala ya UKIMWI kutekeleza majukumu kwa kufuata miongozo,maoni na ushauri unaotolewa na kamati hiyo.

Kauli hiyo amaitoa leo Machi12 ,2023 baada ya Tume ya kudhibiti UKMWI Tanzania (TACAIDS) kuwasilisha Taarifa kuhusu muundo na majukumu yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI katika Ukumbi wa Ofisi za Bunge jijini Dodoma.

Awali akiwasilisha taarifa hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko amesema TACAIDS ni Idara inayojitegemea chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na imeanzishwa kwa mujibu wa sheria Na.22 ya mwaka 2001 na Marekebisho yake Na.6 ya mwaka 2015, sheria hiyo ni kwa ajili ya Tanzania Bara pekee. Zanzibar ipo Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC).

Dkt. Maboko ameyataja majukumu ya TACAIDS kuwa ni kuandaa sera na miongozo kwa ajili ya mwitikio wa UKIMWI nchini pamoja na kusimamia athari zake, kusimamia mpango mkakati kwa ajili ya mipango ya programu za UKIMWI pamoja na masuala mtambuka yahusuyo virusi vya UKIMWI na UKIMWI.

Kujenga mahusiano ya kitaifa na kimataifa kwa watu wote wenye UKIMWI kwa kufanya uratibu wa masuala ya UKIMWI,kutafuta raslimali fedha ,kuzigawa na kuzifuatilia katika programu za Mwitikio wa UKIMWI,kusambaza taarifa kuhusu UKIMWI na madhara yake na programu za kuzuia na kudhibiti.

Kukuza tafiti ,upashanaji taarifa na kutunza kumbukumbu zinazohusiana na udhibiti wa UKIMWI nchini,kukuza uraghibishi na utoaji wa elimu kwa ngazi ya juu kuhusu kuzuia na kudhibiti UKIMWI, kufuatilia na kutathimini shughuli zote za UKIMWI zinazotekelezwa nchini.

Aidha ameongeza kuwa shughuli nyingine ni Kuratibu shughuli zote za UKIMWI na kuzisimamia kwa mujibu wa mkakati wa Taifa wa UKIMWI, kwa kushirikiana na sekta binafsi husika kuwezesha juhudi za upatikanaji wa tiba na kuhamasisha upatikanaji wa tiba na matunzo na chanjo.

Jukumu lingine ni kuhamasisha haki na wajibu kwa watu wanaoishi na VVU ,kuhamasisha WAVIU kuishi kwa matumaini na kushauri serikali kuhusu masuala yote yanayohusu kuzuia na kudhibiti UKIMWI ,kutambua vikwazo katika utekelezaji wa kuzuia na kudhibiti katika sera na programu ,kusimamia shughuli zote zinazohusiana na kuzuia na kudhibiti maambukizi ya VVU na UKIMWI,pamoja na kushirikiana na sekta nyingine husika,kufanya shughuli nyingine za kuzuia na kudhibiti VVU na UKIMWI.

Dkt. Maboko amesema utekelezaji wa majukumu ya TACAIDS unaongozwa na sera ,sheria ,kanuni ,mikakati na miongozo ikiwa ni pamoja na sheria ya tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania Na,22 ya mwaka 2001na marekebisho yake Na6 ya mwaka 2015,Sera ya Taifa ya UKIMWI ya mwaka 2001.

Mwongozo wa uraghibishi na mabadiliko ya tabia,Mwongozo wa VVu na UKIMWI  na magonjwa sugu yasiyoambukiza, mwongozo wa kusshughulikia makundi maalum kuhusu UKIMWI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ,mwongozo wa jinsia na UKIMWI

,Mwongozo wa UKIMWI na haki za binadamu ,Mwongozo wa kufundishia kamati za kudhibiti UKIMWI ngazi za Halmashauri,kata na vijiji, pamoja na mwongozo wa kuunda kamati za kudhibiti UKIMWI kwenye mikoa,mwongozo wa kuunda kamati za kudhibti UKIMWI kwenye Halmashauri.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe Stanslaus Nyongo iliipongeza TACAIDS kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kudhibiti na kupunguza maambukizi ya VVU nchini na kuagiza kuendelea kufanyia kazi ushauri na maekezo yaliyotolewa na kamati hiyo,ikiwa ni pamoja na kufanya ufatiliaji wa utekelezaji wa majukumu ya kamati za kudhibiti UKIMWI ngazi za chini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Stanslaus Nyongo akizungumza na wajumbe pamoja na watendaji wa TACAIDS na Ofisi ya Waziri Mkuu waliohdhuria kikao cha kamati hiyo walipokutana leo jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt Leonard Maboko akiwasilisha Muundo, na Majukumu ya TACAIDS kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI wakati wakikaokilichfanyika leo jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene na Katibu Mkuu Dkt. Jimmy Yonaz (kulia) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt Leonard Maboko alipokuwa anawasilisha Muundo na Majukumu kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Mhe. Seif Salum Seif akichangia wakati wa kikao cha kamati hiyo na TACAIDS kuhusu kubadilisha jumbe zinazotumika kwenye vibao vya ujenzi vinavyo tumia maneno ya Unyanyapaa.

Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya  na masuala ya UKIMWI Mhe Hassan Mtega akichangia wakati wa kikao cha kamati hiyo umuhimu wa TACAIDS kufatilia utekelezaji wa majukumu ya kamati za UKIMWI za ngazi za chini. 

No comments:

Powered by Blogger.