LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkutano wa wadau wa mradi wa Vijana wa Nchi za Maziwa Makuu wafanyika Tanzania

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wadau mbalimbali wa Mradi wa Mtandao wa Vijana wa Nchi za Maziwa Makuu (Great Lakes Youth for Dialogue and Peace), wamekutana jijini Mwanza nchini Tanzania kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na amani.

Mkutano huo wa siku mbili umeanza Alhamisi Mei 25, 2023 ikiwa ni mkutano wa pili wa wadau wa mradi huo nchini Tanzania kufanyika tangu uzinduliwe nchini Juni 30, 2021 ambapo unatekelezwa pia katika nchi za Uganda, DRC Congo, Burundi pamoja na Rwanda.

Wadau hao ni pamoja na viongozi wa dini, jeshi la polisi, mashirika ya kijamii na vijana ambao ni walengwa wakuu ambapo kupitia mradi huo wanapata fursa ya kujadili masuala yanayohamasisha amani katika jamii.

Mradi huo (Great Lakes Youth Network for Dialogue and Peace) unafadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya (European Union), Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la Ujerumani ambapo kwa Tanzania unaratibiwa na taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora (Actions for Democrancy and Local Government- ADLG) ya jijini Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.