LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wananchi Serengeti waandamana, wafunga ofisi, viongozi wajiuzulu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mamia ya wakazi wa Kijiji cha Remung’orori Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, wameandamana hadi katika ofisi ya Serikali ya Kijiji hicho na kuifunga ofisi hiyo. https://youtu.be/QI1-nnD4Jco

Pia wananchi hao wamewashinikiza viongozi wa Serikali ya Kijiji na Chama cha Mapinduzi CCM kujiuzulu wakidai wameshindwa kuwasaidia kutatua mgogoro wa ardhi baina yao na Kijiji jirani cha Mikomariro kilichopo wilayani Bunda.

Wananchi hao wamechukua hatua hiyo Julai 25, 2023 huku pia wakigoma kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo pamoja na kuwazuia watoto wao kwenda shule hadi viongozi wa Serikali ngazi ya Mkoa ama Wizara watakapofika kusikiliza malalamiko yao.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.