LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wakazi wa Kitangiri Mwanza walia na Kituo cha Afya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wakazi wa Mtaa wa Jiwe Kuu Kata ya Kitangiri katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, wameanza maandalizi ya ujenzi wa Kituo cha Afya ambacho kitasaidia upatikanaji wa huduma za afya karibu na kuondoa adha ya kutembea umbali mrefu kusaka huduma.

Wakizungumza wakati wa zoezi la kufanya usafi katika eneo la ujenzi wa Kituo hicho, baadhi ya wakazi hao wamesema kwa sasa wanapata huduma katika Kata jirani hivyo wako tayari kuchangia fedha na nguvu kazi kwa ajili ya ujenzi huo huku wakiomba Serikali kuwaunga mkono.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Jiwe Kuu Kata ya Kitangiri, Patrick Mfungo amesema kukamilika kwa ujenzi wa Kituo hicho cha Afya kutaondoa adha kwa wakazi wa Kitangiri na Kata jirani.

Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Jiwe Kuu, Kandira Mgejwa amesema Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela iko tayari kuunga mkono juhudi za wananchi ili kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo wanayoianzisha.
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA>>> 

No comments:

Powered by Blogger.