Kamati ya Usalama Nyamagana yakagua miradi ya maendeleo
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Ziara hiyo imefanyika Septemba 12, 2023 ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi.
Akizungumza wakati wa kukagua miradi hiyo, Makilagi ameagiza utekelezaji wake kuzingatia mikataba na kuleta thamani halisi ya fedha baada ya kukamilika.
Miradi iliyokaguliwa na Kamati hiyo ni pamoja na mradi wa maji Butimba, jengo la mochwali katika Hospitali ya Butimba, shule mpya ya sekondari Nyamagana, jengo la wagonjwa wa nje, maabara na upasuaji katika Zahanati ya Mkolani, Zahanati mpya ya Sihwa, Zahanati ya Fumagila na shule mpya ya awali na msingi Kanenwa.
Tazama BMG TV hapa chini
Tazama picha hapa chini
SOMA PIA>>> HABARI ZAIDI HAPA
No comments: