LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kilimo cha Vanilla Ununio jijini Dar

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi wa Makampuni ya kimataifa ya kilimo cha Vanilla, Simon Mnkondya amefanya ziara katika shamba la Vanilla lililopo Ununio Beach jijini Dar es salaam.

Ziara hiyo imekuwa yenye matumaini makubwa hasa baada ya kuona kasi ya ukuaji wa vanilla na baadhi ya vanilla kuanza kutoa maua.

"Kwetu Vanilla ni zao lisilo na pingamizi kwenye ukuaji, soko na bila shaka linabakia kuwa zao la kwanza kwa bei kubwa Tanzania na kuwa vanilla ni zao la pili kwa bei kubwa duniani" amesema Mnkondya.

“Hiki kwetu ni kitu kinachotufanya tulipigie debe kubwa zao la vanilla na ikiwezekana kiwe ni kilimo cha Taifa kwa vile zaidi ya 80 ya nchi yetu Tanzania vanilla inamea na kufanya vizuri ikiwa njia za kisasa za Greenhouses na umwagiliaji wa matone zitatumika” ameongeza.

Ameeleza kuwa shamba la Ununio ni shamba lililobezwa sana kwa sababu ya uwepo wa mchanga wa bahari mahali hapo lakini kutokana na umakini wa kampuni ya Vanilla International Limited limekuwa shamba darasa kwa Dar es salaam na maeneo ya jirani.

No comments:

Powered by Blogger.