LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mahafali ya 12 chuo cha ufugaji nyuki Tabora yafana

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imewataka wahitimu wa sekta ya nyuki wa chuo cha mafunzi ya ufugaji nyuki Tabora (BTI), kuwa wabunifu na kutumia fursa zilizo katika mnyororo wa zao hilo ili kujiajiri.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mafunzo na Utafiti wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Edward Kohi ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu katika mahafali ya 12 ya chuo hicho ambapo amesema Wizara itaendelea kutoa nafasi za ajira kwa kadri upatikanaji wa vibali vya kufanya hivyo.

"Kinachotakiwa ni kuwa wadadisi wa fursa zilizopo katika mnyororo mzima wa thamani katika sekta ya ufugaji nyuki, Nina imani hamuwezi kukosa nafasi katika mnyororo huu" amesema Dkt. Kohi

Aidha Dkt. Kohi amesema mpaka sasa Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi na kuwajengea uwezo wadau mbalimbali katika kusimamia rasilimali za nyuki na kuendelea kukuza mchango wake katika pato la taifa ikiwa ni pamoja na kukuza uzalishaji wa mazao ya nyuki nchini.
.
Amesema Serikali imeanzisha mkakati wa wananchi wote kuachia shoka na kukakamata mzinga lengo ikiwa ni kuboresha sekta ya ufugaji nyuki hivyo wahitimu hao watumie fursa hiyo kubuni na kuanzisha kampuni za kufanya biashara ya ufugaji nyuki.

"Wizara inaendelea na Mkakati wake nchi nzima wa kuachia shoka na kukamata mzinga, Tumieni fursa hii kuanzisha kampuni za kuwasaidia kufanya biashara katika sekta ya ufugaji nyuki" amesema Dkt. Kohi

Ameongeza kuwa serikali inaendelea kubuni mbinu mbalimbali za kukuza sekta ya misitu na nyuki na kuendelea kuboresha mnyororo wake wa thamani ili kila mshiriki katika mnyororo huu uweze kufaidika.

"Nia ya serikali ni kukuza sekta ya misitu na nyuki ili iweze kuleta tija zaidi, Hivyo niendelee kuwatia moyo kuwa serikali ina nia njema ya kukuza na kusimamia seka hii ya ufugaji nyuki".

Dkt. Kohi ameongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii lengo lake kuu nikuona vyuo mbalimbali vilivyopo chini ikiwemo Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki (BTI) kinatoa elimu bora ikiwemo kuwa na waalimu wenye weledi katika sekta hiyo.

Amesema lengo lingine nikuhakikisha vyuo hivyo vinatengeneza mahusiano na Taasisi mbalimbali za nje ili kuongeza uelewa na weledi.

Amewataka wakazi wa Tabora kujiandaa na kongamano lijalo la Ufugaji nyuki la "Apimondia" linalo tarajia kufanyika mwaka 2027 kutengeneza fursa za kujipatia kipato kupitia kongamano hilo

Ameongeza kuwa katika kutatua changamoto za malazi katika chuo hicho, Wizara kupitia Mradi wa BEVAC imepanga kujenga Bweni la wanafunzi wa kike mia tatu (300) huku Bweni la Wavulana likiwa katika mkakati pia.

Kwa Upande wake Mkuu wa Chuo Cha Mafunzo cha Ufugaji Nyuki ( BTI), Semu Daud amesema jumla ya wahitimu waliyohitimu chuoni hapo ni 243 ambapo kwaupande wa Shahada jumla ni wahitumu 114 na Astashahada ni wahitimu 129.
Na John Bera, Tabora

No comments:

Powered by Blogger.