LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wananchi watakiwa kuzingatia elimu ya fedha kabla ya kukopa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Meneja Masoko na Uhamasishaji wa Mfuko wa Self Microfinance Fund uliopo chini ya Wizara ya fedha Linda Mshana akiongea na waandishi wa habari katika Maonyesho ya tatu ya wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa yanafanyika mkoani Arusha, kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abed Jijini, Arusha.
Afisa mikopo kutoka Self Mbwana Msangule akiendelea kuwapa elimu wateja waliouthuria katika banda lao lililopo katika Maonyesho

Na Woinde Shizza, Arusha
Ili kuepuka matatizo ya kuuziwa mali , kutokana na kushidwa kurejesha mikopo wanayochukuwa katika taasisi mbalimbali watanzania wametakiwa kujitokeza Kwa wingi kupata elimu itakayowasaidia kutimiza malengo yao ambayo yatasaidia kukuza uchumi wao pamoja na nchi Kwa ujumla.

Aidha pia kutokuwa na uelewa wa kutosha pamoja na elimu ya duni ndio chanzo pekee kinachopelekea baadhi ya watanzania kushidwa kurejesha mikopo mbalimbali kwani watu wengi wamekuwa wakifanya maamuzi pasipo kuwa na uelewa wa kutosha katika eneo hilo

Hayo yamebainishwa na Meneja Masoko na Uhamasishaji wa Mfuko wa Self Microfinance Fund uliopo chini ya Wizara ya fedha Linda Mshana wakati akiongea na waandishi wa habari katika Maonyesho ya tatu ya wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa yanafanyika mkoani Arusha, kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abed Jijini, Arusha ambapo alisema kuwa

mfuko huo umelenga kukidhi mahitaji ya mikopo kwa makundi mbalimbali Tanzania

Amesema kuwa kumekuwa na tatizo la wananchi wengi kuchukua mikopo bila kupata elimu ya kutosha ya namna ya kurejesha mikopo hiyo ,asilimia wanayopaswa kurejesha na namna ya kutumia mikopo hiyo katika lengo kusudiwa.
Amesema kuwa mfuko huo wa SELF pia unasaidia kutatua matatizo ya wananchi katika mahitaji ya msingi katika kukuza ujasiriamali, biashara, Kilimo ,Ufugaji vilevile hatakupata makazi na kuwekeza kwenye viwanda.

Amebainisha kuwa kulingana na mahitaji ya mikopo na kuongezeka kwa utitiri wa taasisi za mikopo,vijana wa kitanzania wanashauriwa kuungana na kukopa kwenye taasisi za fedha za kuaminika na zenye usimamizi wa serikali ili kuepuka fedhea katika mikopo hiyo huku akiwasihi kupata elimu ya kutosha kabla ya kuichukuwa mikopo hiyo .

Ametaja aina za mikopo ambazo zinatolewa na mfuko wa SELF Microfinance ni pamoja na mkopo wa Kilimo,Biashara, Makazi,mkopo wa Pamoja, mkopo wa Imarika, Mkopo wa Mahitaji na mikopo wa Mkulima ambapo pia alifafanua kuwa nia yao ni kuendela kuwapatia watanzania elimu na kuchangamkia fursambalimbali zilizopo hapa nchini.

Amesema kila mtanzania ana fursa kubwa ya kupata mkopo na kujikuza kiuchumi, kwa wajasiriamali wote wachini, wa kati, wakubwa, wafanyakazi na watuwanaotaka kuboresha makazi

“Wale waliopo kwenye vikundi wanaotaka mikopo ya kujiinua kiuchumi, wasiache fursa zikawapita, tunawafanyakazi waliokidhi na wana weledi wakuhudumia wajasirimali wote wanaotaka kujinua kichumi wafike tu katika matawi yetu yalipo katika mikoa mbalimbali ikiwemo hapa Arusha katika jengo la hazina ,Mwanza ,Dodoma,Dar es salaam ,mbeya, kahama ,Geita, Morogoro,Tanga ,Mtwara, Iringa pamoja na Zanzibar kupata elimu ya kutosha kuhusiana na mikopo namna ya kurejesha pamoja na riba" amebainisha Linda.

No comments:

Powered by Blogger.