LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanaharakati wa jinsia watakiwa kuwa sauti ya wanyonge

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi amewataka wadau wanao hudhuria mafunzo ya semina za jinsia na maendeleo(GDSS) kuwa watetezi wa kwanza katika kupigania usawa Kijinsia na kukemea vitendo vya ukatili hadharani kutokana na yale wanayo jifunza.

Ameyasema hayo Disemba 15, 2023 Mabibo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanaharakati wa jinsia katika ofisi za mtandao wa Jinsia nchini amesema anatamani akiona mtu aliye alikwa na kuhudhuria semina hizo Mara kwa mara akiwajibika kwa vitendo katika utetezi wa masuala yenye mlengo wa Kijinsia ili kuleta matokeo chanya ya semina hizo.

"Natamani kila anaye kuja hapa atoe hesabu ya kile alicho jifunza amefanyia nini amegusa maisha ya watu wangapi sio suala la kwenda Dar es saalam tusipoteze wakati huu kwani ni rasmali ya nchi,na pesa zinazo tumika kufanya mikutano hii ni nguvu za walipa Kodi wa nchi fulani na serikali yetu imeweka mkono wake wanatamani waone yale tulisema tutayafanya" Liundi amesema.

Aidha ameeleza kuwa wanapaswa kuleta mrejesho wa nini kimefanyika katika vipindi tofauti tofauti kwa wale watu ambao Wana uhitaji wa taulo za kike mashuleni,wanao fanyiwa ukatili sehemu mbalimbali ambapo itaonesha kwa namna gani wametoa elimu.

Kwa upande wake, naye muwakilishi wa Idara ya uwezeshaji na Mafunzo,Bi Lina Sangai amesema kuwa wametoa mafunzo ambayo ni muendelezo wenye lengo la kutambua nini wamepata kujifunza wanapokua wakifundisha watu wengine na changamoto wanazo zipitia wakati wakitoa mafunzo ili kutatua changamoto zitakazo jitokeza

Naye Mwanaharakati wa jinsia kutoka mkoa wa Mara, Wilaya ya Tarime Bi.Noela Joseph amesema kuwa ametumia muda wake kutoa elimu kwa jamii inayo mzunguka ili wanapojitambua na changamoto zitakapo jitokeza wapate sehemu ya kukimbilia.

"Kuna mtoto aliozwa akiwa na umri mdogo kwa maana alikua ni mwanafunzi wakataka kumkatiza ndoto zake baada ya matokeo kuwa yametoka amefaulu lakini wazazi walikua wameshapokea mahali lakini huyo mtoto tuliweza kupata taarifa na kumnusuru amerudi shule na mpaka sahivi anaendelea na shule" Noela amesema.

Mafunzo hayo yaliyo andaliwa yana kwenda kuwapatia wakufunzi uwezo ambao watakwenda kutoa mafunzo katika mikoa mikoa nane ya Tanzania kwa wanaharakati walio katika vituo vya taarifa na yanafanyika kwa ushirikiano na taasisi ya Global affairs Canada.

No comments:

Powered by Blogger.