LIVE STREAM ADS

Header Ads

Tanzania kunufaika na miradi ya mabadiliko ya tabianchi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Desemba 18, 2023 kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) uliofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Na Emmanuel Mbatilo, Dar 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo amesema Tanzania inatanufaika na fedha za miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Ametoa kauli hiyo Desemba 18, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) uliofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Dkt. Jafo amesema kupitia mkutano huo uliofanyika Novemba 30 hadi Desemba 12, 2023 Tanzania inatarajia kunufaika na teknolojia na Programu ya Afrika ya Nishati Safi ya Kupikia pamoja na afya.

Amesema kuwa programu hiyo inaunga mkono juhudi za Serikali za kuhamasisha kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ambayo yanasababishwa na ukataji wa miti.

Pamoja na manufaa hayo, Waziri Jafo amesema kuwa pia utekelezaji wa mikakati ya kuimarisha uhimili katika katika sekta ya maji, misitu na bahari ambayo ni mojawapo ya rasilimali muhimu kwa uchumi wa buluu.

“Katika mkutano wa COP28 wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania walikutana na wenzao kutoka nje ya nchi na kujadiliana kuhusu fursa za uwekezaji kwenye eneo la mabadiliko ya tabianchi ambapo jumla ya taasisi na kampuni zaidi ya 56 zimeonesha nia ya kuwekeza nchini kwa kushirikiana na sekta binafsi nchini” amesema Dkt. Jafo.

Halikadhalika amebainisha kuwa katika kuwezesha ushiriki kikamilifu, Tanzania iliandaa msimamo wa taifa uliosaidia kuongoza dira ya ushirikiri na majadiliano ya wajumbe wa Tanzania, ulioandaliwa kwa ushirikianao na wadau mbalimbali.

Aidha, Dkt. Jafo ameongeza kuwa ujumbe wa Tanzania ulikuwa ni ‘Kuimarisha Hatua za Kilimo Himilivu na Uchumi wa Bluu’, iliyolenga kuchochea hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa na kilimo endelevu na kutumia vizuri fursa za uchumi wa buluu.

Hivyo, mkutano wa 29 (COP 29) umepangwa kufanyika nchini Azerbaijan kuanzia Novemba 11 hadi 22, wakati COP30 itafanyika nchini Brazil kuanzia Novemba 10 hadi 21, 2025.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 18, 2023 kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) uliofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 18, 2023 kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) uliofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
Baadhi ya watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakifuatilia Mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Desemba 18, 2023 kuhusu ushiriki wa Tanzania katika mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) uliofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

No comments:

Powered by Blogger.