LIVE STREAM ADS

Header Ads

TBS, BRELA na WMA zatakiwa kufanya ukaguzi kwenye viwanda vya mabati

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt, Ashatu Kijaji (MB) amezitaka Taasisi zinazohusika na utoaji Leseni(BRELA) Shirika la Viwango Tansania (TBS) na wakala wa vipimo sahihi (WMA)kupita kwenye viwanda vyote nchini vinavyozalisha bidhaa za mabati na bidhaa nyingine kukagua na kujiridhisha kama bidhaa zinazozalishwa na viwanda nchini zinakidhi vigezo vilivyo vilivyoainishwa na kukubalika na Serikali.

Waziri Kijaji ameyasema hayo 22 Febriari, 2024 jijini Dodoma wakati alipofanya ziara katika Viwanda vya kuzalisha mabati vya ALAF na Herosean Interprises inayozalisha mabati ya DRAGON ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa na Viwanda hapa nchini zinanoreshwa.

Aidha Mhe. Waziri akiwa kwenye kiwanda cha Herosean Interprises kinachozalisha mabati ya DRAGON ameweza kubaini uwepo wa bidhaa nyingine ambazo haziusiani na malengo halisi ya leseni iliyotolewa na BRELA.

"Leo nimetembelea Viwanda hivi viwili lakini cha kusikitisha hiki Kiwanda cha kuzalisha mabati ya DRAGONI kinajihusisha na biashara ya kuuza bidhaa nyingine ikiwemo Friji, PVC, Vigae na Gypsum bord ,

"Nimewataka wanioneshe vielelezo vya usajili wa bidhaa hizo tofauti na bidhaa za mabati kiwandani hapa,sikupata majibu sahihi , naziagiza taasisi zinazohusika na hili suala zilishughurikie ili kupata ukweli wake. Amesema Kijaji

Vile vile Waziri Dkt.Kijaji ametoa wito kwa Viwanda vinavyozalisha bidhaa za mabati hapa nchini kuuzwa kwa bei rafiki ili kunufaisha wanunuaji kwa makundi yote.

" Jambo lingine ninalotaka kuwaambia watanzania kwa bidhaa nilizotembelea leo ,ukilinganisha kwa nchi za Afrika mashariki kwa bidhaa hii ya mabati sisi Tanzania bei yetu ipo chini kuliko nchi yoyote ile ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo niwatake msisikilize kelele za mtaani endeleeni kujenga kwa wingi na sisi kama Serikali tunaendelea kutekeleza miradi yetu" ameongeza Dkt. Kijaji.

Kwa nyakati tofauti, wazalishaji wa viwanda hivyo Herry Jailos afsa huduma kwa wateja kiwanda cha mabati ya Alaf na Boniface Lekwasa Afsa Masoko Kiwanda cha kuzalisha mabati Dragon

wameishukuru Serikali kufanya ziara na kubaini changamoto zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa masoko kutokana na wazalishaji wa bidhaa hizo kuwa wengi nchini.

No comments:

Powered by Blogger.