LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Makalla afanya mazungumzo na wanahabari Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla amefanya mazungumzo na waandishi wa habari kwa lengo la kuimarisha ushirikiano zaidi.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Februari 23,2024, RC Makalla ameridhia kuwa mlezi wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC) huku akiahidi kuchangia pikipiki mbili kwa chama hicho kwa ajili ya kuanzisha mradi wa kiuchumi wa usafirishaji (kukodisha kama bodaboda).

Pia ameahidi kuratibu harambee kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ofisi za MPC katika eneo la Kisesa nje kidogo ya Jiji la Mwanza huku akitumia mazungumzo hayo kuwahimiza waandishi wa habari kuendelea kutangaza vivutio vya utalii pamoja na miradi ya kimkakati mkoani Mwanza.

Awali Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko alisema waandishi wa habari na vyombo vya habari wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo maslahi dunia kutokana biashara ya matangazo kuyumba.

Kuhusu Sheria tata zinazosimamia waandishi wa habari na vyombo vya habari, Soko alisema MPC inaendelea kuwajengea uwezo wanachama wake ili kutokizana na Sheri hizo wakati mazungumzo na mijadala mbalimbali ya kuzirekebisha ikiendelea.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA SOMA>>> HABARI ZAIDI HAPA

No comments:

Powered by Blogger.