LIVE STREAM ADS

Header Ads

Dkt. Biteko afungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Nishati

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akilakiwa na viongozi mbalimbali wakati akiwasili katika ukumbi wa hoteli ya Malaika jijini Mwanza kwa ajili ya kufungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati unaofanyika kwa siku mbili kuanzia Jumatatu Machi 18, 2024.

Baraza hilo hilo la tano linatarajia kujadili masuala mbalimbali ikiwemo ikama na bajeti ya mishahara kwa mwaka 2024/25 na bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2024/25.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akiwasili katika ukumbi wa hoteli ya Malaika jijini Mwanza kwa ajili ya kufungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati unaofanyika kwa siku mbili kuanzia Jumatatu Machi 18, 2024.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akiwa n viongozi mbalimbali meza Kuu wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati unaofanyika jijini Mwanza.
Akifungua mkutano huo, Dkt. Biteko amewahimiza viongozi wa Wizara ya Nishati kuwaunganisha wafanyakazi badala ya kuwa chanzo cha kuwagawa makundi makundi.

"Unaonaje fahari kuabudiwa na kutukuzwa kwa sababu ya cheo ambacho ni cha muda tu" amehoji Dkt. Biteko.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG 

No comments:

Powered by Blogger.