Dkt. Biteko aweka jiwe la msingi mradi wa umeme jua Kishapu, Shinyanga
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa mradi wa umeme jua, unaotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo katika eneo la Ngunga Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Hafla ya uwekaji jiwe hilo imefanyika Alhamisi Machi 14, 2023 na kuhudhuriwa pia na wananchi, wadau na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Serikali.
Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Biteko amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi huo, kampuni ya Sinohydro kutoka nchini China kukamilisha kazi kwa wakati ili kuondoa adha ya uhaba wa umeme kwa wananchi.
"Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan anakwerwa na adha ya umeme kukatika ndiyo maana ametuagiza kufanya kazi kuhakikisha wananchi wanapata umeme" amesema Dkt. Biteko akibainisha kuwa Serikali inatekeleza miradi ya nishati mbadala ikiwemo umeme jua Kishapu, joto ardhi Songwe na Mbeya ili kukabikiana na uhaba wa umeme.
Dkt. Biteko amesema baada ya mtambo wa kwanza wa kuzalisha umeme kuwashwa katika mradi wa bwawa la Mwl. Julius Nyerere, pia mitambo mingine miwili inatarajiwa kuwashwa mwezi ujao na kusaidia uzalishaji wa umeme KW 400.
Dkt. Biteko ametoa rai kwa wananchi na watumiaji wa nishati ya umeme kuilinda miundombinu ya umeme kwani suala la uzalishaji wa umeme linaendana na kutunzaji wa miundombinu inayosafirisha umeme kwenda kwa wananchi.
Katika hatua nyingine Dkt. Biteko amewataka wateja zikiwemo taasisi za umma wanaodaiwa na Shirika la umeme TANESCO kulipa madeni yao kwani hakuna haki ya kudai umeme kama hakuna wajibu wa kulipa madeni hayo.
Pia Dkt. Biteko amewatataka watumishi wa Wizara ya Nishati ikiwemo TANESCO na REA kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali watatue kero za wananchi ambapo amewata viongo wa REA mkoani Shinyanga kueleza kwa nini hawakuhudhuriwa hafla hiyo na hivyo kushindwa kupata ufafanuzi wa changamoto ya usambazaji umeme Vijijini iliyowasilishwa kwake.
Alitoa taarifa kuhusu mradi huo, Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji Umeme (TANESCO), Mhandisi Coastal Rubagumya aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji TANESCO amesema jumla ya KW 150 zinatarajiwa kuzalishwa baada ya mradi huo kukamilika.
Amesema gharama za mradi huo ulioanza Disemba 2023 ni bilioni 323 ikiwa ni fedha za wadau Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFDA) pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo mradi unatarajiwa kukamilika Januari 2025.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la mradi wa umeme jua Kishapu mkoani Shinyanga ambapo amepongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara barani Afrika katika kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ili kukabikiana na changamoto za kimazingira.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la mradi wa umeme jua Kishapu mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Joseph Mkude alitoa salamu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga ambapo amesema mradi wa umeme jua Kishapu unasaidia kuchochea shughuli za kimaendeleo wilayani humo.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akisalimiana na wakati wa Kishapu.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kishapu, Mwl. Emmanuel Johnson pamoja na viongozi mbalimbali.
Meneja wa mradi wa umeme jua Kishapu (kulia) alitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi huo.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko (kushoto) akitoa maelekezo kwa mwakilishi wa kampuni ya Sinohydro mradi wa umeme jua Kishapu mkoani Shinyanga.
Meneja wa mradi akitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa mradi wa umeme jua Kishapu.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko (kushoto) akitoa maelekezo kwa mwakilishi wa kampuni ya Sinohydro mradi wa umeme jua Kishapu mkoani Shinyanga.
Mwonekano wa 'SITE' kwenye mradi wa umeme jua Kishapu mkoani Shinyanga.
Mwonek utekelezaj Kishapu.
Mradi wa umeme jua Kishapu mkoani Shinyanga unaratajia kuimarisha upatikanaji wa nishati ya umeme katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na Mara.
No comments: