JUMIKITA, TAHLISO waandaa kongamano kubwa Dar
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi Mei 18,2024, Mwenyekiti JUMIKITA, Shaaban Matwebe amesema kongamano hilo linalotarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 500, litaongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa.
"JUMIKITA inapenda kuutaarifu umma kuwa, kongamano hilo litakuwa na dhima kuu ya kujadili uandishi wa habari kupitia mitandao ya kijamiii pamoja na upashanaji wa habari kupitia mitandao hiyo" amesema Matwebe na kuongeza;
"Pamoja na dhima hiyo kuu, kongamano hilo pia litajadili mafanikio ya miaka mitatu ya JUMIKITA, miaka mitatu ya Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan na maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani" amesema Matwebe na kuwakaribisha wadau mbalimbali kwenye kongamano hilo muhimu.
Ameongeza kuwa mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii na uzalendo, fursa zilizopo kwenye tasnia hii, mafanikio na changamoto ili kutoa mchango wa kiundeshaji kwa wadau kupitia JUMIKITA na mapendekezo yatakayosaidia Serikali kwenye uratibu wa Sera za jinsi ya kuunganisha sayansi ya uchumi wa taarifa (information economics) na uchumi wa taarifa (information economy).
Mawasiliano: Mwenyekiti JUMIKITA, Shaaban Matwebe 0717073534
Sekretarieti: Dickson Frank Mushi 0686379370
No comments: