Hafla ya kuipongeza timu ya Chuo cha Misungwi CDTTI
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Uongozi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi (Misungwi CDTTI) mkoani Mwanza, umeandaa hafla ya kuipongeza timu ya soka ya chuo hicho baada ya kuibuka mshindi wa tatu kwenye michuano ya Tigo Chuo Challenge Cup 2024.
Halfa ya kuipongeza timu hiyo imefanyika Jumamosi Juni 29, 2024 majira ya jioni ikitanguliwa na michezo mbalimbali (Sports Bash 2024) ikiwemo jogging iliyofanyika majira ya asubuhi pamoja na soka iliyohusisha wanafunzi pamoja na waalimu wao majira ya alasiri.
Katika mchezo wa kwanza wa soka, timu ya wanafunzi wa kike Level Four imeibuka na ushindi wa goli moja kwa nunge dhidi ya timu jumuishi ya Level Five na Six, timu ya soka ya chuo imebuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya timu ya mashabiki wa chuo huku wafanyakazi wa chuo (Staff) wakiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya timu ya Serikali ya wanafunzi.
Mkuu wa chuo hicho, Arch. Charles Achuodho alisema mbali na masuala ya kitaaluma, pia chuo hicho kimelenga kuendeleza vipaji mbalimbali vya wanafunzi ikiwemo soka na hivyo kutoa rai kwa wachezaji kujiandaa vyema ili mashindano yajayo wafike hatua ya fainali.
"Wengine wamejiuliza kama mshindi wa tatu anapongezwa kwa sherehe namna hii, tukichukua kombe itakuwaje, nami nasema itakuwa zaidi ya hapa na hata viongozi wetu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum watatamani kufika" alisema Achuodho.
Naye Makamu Mkuu wa chuo hicho upande wa taaluma, Dongo Nzori alisema lengo la kuwapongeza wachezaji hao ni kuwapa morari wa kufanya vizuri zaidi katika michezo huku wakijiimarisha kiafya hatua itakayowasaidia pia kuzingatia masomo yao.
Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo, Mratibu wa Tigo Chuo Challenge Cup, Dickson Mpilipili aliwapongeza wachezaji na uongozi wa chuo cha Misungwi CDTTI kwa kuibuka nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo ikiwa ni mara yao ya kwanza kushiriki.
Michuano ya Tigo Chuo Challange Cup msimu wa tatu ilifanyika katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza kuanzia Aprili 27, 2024 hadi Juni 09, 2024 ikishirikisha vyuo 32 ambapo ubingwa ulienda kwa chuo cha Mipango, mshindi wa pili chuo cha SAUT na Misungwi CDTTI mshindi wa tatu ambapo michuano hiyo huandaliwa na mwandishi wa habari za michezo, Dickson Mpilipili.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Timu ya wafanyakazi Chuo cha Misungwi CDTTI.
Timu ya Serikali ya wanafunzi Misungwi CDTTI.
Mchezo kati ya wafanyakazi wa Misungwi CDTTI na Serikali ya wanafunzi Misungwi CDTTI umekuwa wa kuvutia.
Mchezaji wa timu ya Serikali ya wanafunzi Misungwi CDTT akifanya shambulizi langoni mwa timu ya wafanyakazi Misungwi CDTTI.
Mtangazaji/ mwanahabari Dickson Mpilipili (kushoto) akimpongeza Makamu Mkuu wa Chuo cha Misungwi CDTTI upande wa Taaluma, Dongo Nzori (kulia).
Timu ya wafanyakazi Misungwi CDTTI ikifanya shambulizi.
Timu ya wafanyakazi Misungwi CDTTI ikifanya shambulizi.
Mashabiki wakifuatilia soka.
Wachezaji wa timu ya wafanyakazi Misungwi CDTTI wakipongezana kwa ushindi.
Wachezaji wa timu ya wanafunzi na wafanyakazi wa Misungwi CDTTI wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Wachezaji wa timu ya wafanyakazi Misungwi CDTTI wakitoka uwanjani kifua mbele kwa ushindi wa goli 1-0 shidi ya timu ya Serikali ya Wanafunzi Misungwi CDTTI.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: