LIVE STREAM ADS

Header Ads

Pamba Jiji FC yaendelea kufungua matawi mapya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, James Chuwa amezindua tawi la timu ya Pamba Jiji FC lililopo Ngudu wilayani humo.

Zoezi hilo limeambatana na uuzaji wa tiketi kwa ajili ya Pamba Day, uuzaji wa jezi na mchezo kati ya timu ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba iitwayo KWIDICO Junior na timu ya MODO SC inayoongozwa na mdau wa michezo wilayani Kwimba.

Timu ya hamasa wilayani Kwimba imeongozwa na Afisa Michezo Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mohamed Bitegeko ambapo tayari hamasa kama hiyo imefanyika wilayani Ukerewe na itaendelea katika Wilaya zote za Mkoa Mwanza kuelekea kilele cha Pamba Day Agosti 10, 2024 katika uwanja wa CCM Kirumba.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.