Kibaha yaahidi kuendelea kufanya kweli utunzaji wa mazingira
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, Nickson Simon amesema Wilaya hiyo itaendelea kutenga bajeti ya utunzaji na usafi wa mazingira.
"Sisi kama Wilaya ya Kibaha,tunafanya kweli katika usafi wa Mazingira ambapo kama Halamshauri huwa tunatenga bajeti ya usafi. Pia tumefanikiwa kutenga bajeti ya nishati safi" alisema.
Alizishauri pia familia ziweze kutenga bajeti ili kufanya kweli katika kununua pedi za watoto wa kike na wasibaki nyuma katika hedhi salama.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Salum Ally alisema upande wa nishati safi hawajabaki nyuma kwakuwa Halmashauri yao huwa inawapa wakazi wake majiko ya gesi kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati.
Aliwaomba pia wazazi wasibaki nyuma katika kuwafundisha watoto wao kuhusu hedhi salama. Ally alisema pia huwa wanafanya kampeni
"Hedhi salama sio siri, ni wakati sasa wazazi kuacha kuona aibu bali wanatakiwa kuwafundisha watoto wao jinsi ya kutumia pedi pamoja na kuzihifadhi pedi hizo katika chombo malumu ili wasichafue mazingira" alisema.
No comments: