LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia afanya makubwa Kiteto mkoani Manyara

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mbunge wa Jimbo la Kiteto mkoani Manyara, Edward Ole Lekaita amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi kwa wakati.

Lekaita alisema Rais Samia amekuwa kinara kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo ambapo ametaja mafanikio ya miradi mbalimbali ikiwemo kampeni ya kumtua ndoo mama kichani ambapo upatikanaji wa maji safi na salama katika jimbo la Kiteto umeongezeka.

Mbunge huyo alitoa pongezi hizo tarehe 07 Septemba 2024 wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Ndirigishi baada ya kuzindua shule mpya ya sekondari Ndirigishi.
Alisema kuwa kwa mafanikio ya miradi mbalimbali Rais Samia anaenda kuandika historia kubwa katika jimbo la Kiteto na nchi kwa ujumla wake.

Alisema kuwa katika uongozi wa Rais Samia, shilingi bilioni moja zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule na mabweni katika shule hiyo ya sekondari Ndirigishi, bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa Chuo vya Ufundi Stadi (VETA) wilaya ya Kiteto, Bilioni moja kwa ajili wa ujenzi wa soko la mazao Engusero na bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.

Mbunge Ole Lekaita alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukamilisha upatikanaji wa umeme katika vijiji vyote katika Wilaya ya Kiteto, pia alisema zaidi ya madarasa 200 yamejengwa katika kipindi cha uongozi wake huku shule shikizi 18 pia zikijengwa na kusajiliwa huku ahule mpya mbili za msingi zikiwa zimejengwa katika Kata ya Matui na Dongo.

No comments:

Powered by Blogger.