CRDB Yatoa Mafunzo kwa Mawakala Shinyanga
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Bw. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati akifungua mafunzo maalum kwa Mawakala wake kutoka Mkoa wa Shinyanga

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Benki ya CRDB imeendesha mafunzo maalum kwa Mawakala wake kutoka Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuwaongezea uelewa na ufanisi katika utoaji wa huduma bora za kibenki kwa wananchi.
Mafunzo hayo yamefanyika leo Jumatatu Juni 23,2025 katika Ukumbi wa Makindo Hotel, Mjini Shinyanga yakihusisha mada mbalimbali muhimu ikiwemo, Utoaji wa huduma bora kwa wateja, Huduma mbalimbali za kibenki, Udhibiti wa utakatishaji fedha na elimu ya ujasiriamali ili kukuza biashara za mawakala.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Bw. Jumanne Wambura Wagana, amewahimiza Mawakala hao kuwa mabalozi wa huduma bora na waaminifu kwa jamii, akisisitiza kuwa wao ni kiungo muhimu kati ya benki na wananchi waliopo katika maeneo ya vijijini na mjini.
“Kazi za Uwakala zinahitaji umakini na uaminifu. Tuendelee kuchukua tahadhari wakati wa kutoa huduma kwa sababu matukio ya wizi wa kutumia nguvu na utapeli mtandaoni yanaongezeka. Epukeni rushwa na vitendo vya utakatishaji fedha,” amesema Wagana.
Aidha, amewashauri Mawakala kuimarisha usalama wa ofisi zao na kukata bima ya fedha ili kujikinga dhidi ya hasara zinazoweza kujitokeza kutokana na biashara ya fedha au miamala.
Ameeleza kuwa, Benki ya CRDB inaendelea kuhakikisha kuwa, huduma zake zinafika kwa wananchi wote kwa ufanisi na kwa kuzingatia usalama wa kifedha.
Kwa upande wake, Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB Kanda – Kitengo cha Mawakala, Bw. Kidagaa Kubalunga, amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa CRDB kuhakikisha kila wakala anatoa huduma bora kwa kuzingatia maadili ya kazi, maarifa ya kifedha na matumizi ya teknolojia.
“Tunataka kila CRDB Wakala awe na uelewa mpana kuhusu huduma za benki, udhibiti wa miamala yenye viashiria vya utakatishaji fedha na pia awe na uwezo wa kuwahudumia wateja kwa njia rafiki, salama na ya kisasa,” amesema Kubalunga.
“Tunayatambua mafanikio makubwa yanayotokana na mtandao wa mawakala nchini. Hawa ndiyo wanaosogeza huduma za kibenki hadi maeneo yasiyofikika na matawi ya benki,” ameongeza.

Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Bw. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati akifungua mafunzo maalum kwa Mawakala wake kutoka Mkoa wa Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Bw. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati akifungua mafunzo maalum kwa Mawakala wake kutoka Mkoa wa Shinyanga

Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Bw. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati akifungua mafunzo maalum kwa Mawakala wake kutoka Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Bw. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati akifungua mafunzo maalum kwa Mawakala wake kutoka Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Bw. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati akifungua mafunzo maalum kwa Mawakala wake kutoka Mkoa wa Shinyanga
Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB Kanda – Kitengo cha Mawakala, Bw. Kidagaa Kubalunga akizungumza wakati wa mafunzo maalum kwa Mawakala wake kutoka Mkoa wa Shinyanga
Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB Kanda – Kitengo cha Mawakala, Bw. Kidagaa Kubalunga akizungumza wakati wa mafunzo maalum kwa Mawakala wake kutoka Mkoa wa Shinyanga
No comments: