LIVE STREAM ADS

Header Ads

Dida achukua fomu ya ubunge Viti Maalum Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa anayewakilisha Mkoa wa Mwanza, Khadija Mfaume Liganga (Dida) amechukua fomu kuomba ridhaa ya kuwania ubunge wa Viti Maalum Wanawake katika Mkoa wa Mwanza.

Mbali na nafasi yake ndani ya UWT, Dida pia anajulikana kama mwanaharakati mahiri wa haki za wanawake. Amekuwa akiandaa na kuratibu makongamano mbalimbali na pia ni muandaaji wa Tuzo Maarufu za Mwanamke Kinara zinazotolewa Kanda ya Ziwa.

No comments:

Powered by Blogger.