LIVE STREAM ADS

Header Ads

Masha akitosa tena ubunge Nyamagana

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Lawrence Masha ni miongoni mwa wanachama wa CCM waliochukua fomu ya kuwania ubunge jimboni humo.

Masha ambaye pia amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne, amekoleza joto ya uchaguzi katika Jimbo la Nyamagana ambalo watia nia wengi akiwemo mbunge wa sasa Stanslaus Mabula wamechukua fomu kwa 'style' ya kimya kimya tofauti na ilivyoonekana katika majimbo mengine nchini.

Lawrence Masha alikuwa Mbunge wa Nyamagana (2005- 2010), Naibu Waziri wa Nishati na Madini (2006), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (2006- 2008) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (2008- 2010).

Safari ya Masha 2025
Imeandaliwa na Nashon Kennedy, Mwanza

Mbunge wa zamani wa Jimbo la Nyamagana, Lawrence Kego Masha ni miongoni mwa wanachama wa CCM waliojitokeza leo kuwania ubunge katika Jimbo la Nyamagana.

Amesema ameamua kujitosa kuwania nafasi hiyo kwa madai kuwa uwezo wa kuongoza anao na kwamba jimbo la Nyamagana ni nyumbani kwao.

Amesema wakati akiwa Mbunge wa Jimbo hilo la Nyamagana alifanya mambo makubwa ya kimaendeleo ikiwemo uboreshaji wa miundombinu na shughuli nyingine za kiuchumi.

Aidha amesema yeye kama kijana bado ana uwezo mkubwa wa kuongoza na yuko tayari kuwatumikia wakazi wa Nyamagana.

"Nina uwezo na dhamira ya kuendelea kuwatumikia wana nyamagana ili niweze kutimiza na kutekeleza mambo ya kimaendeleo na ni tumaini wana Nyamagana wataniunga mkono" amesema Masha.

No comments:

Powered by Blogger.