LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mme auawa na mkewe kwa tuhuma za wivu wa mapenzi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamsaka mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Mgore (25), mkazi wa Kirumba, Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza kwa tuhuma za mauaji ya mume wake aitwaye Amosi Paulo (31) ambaye ni dereva pikipiki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, tukio hilo linadaiwa kutokea tarehe 25.06.2025 baada ya mwanamke huyo kudaiwa kumpiga mmewe na kitu chenye ncha kali eneo la shingoni na hivyo kumsababishia kifo majira ya 4:30 usiku, muda mchache baada ya kufikishwa katika hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-Toure kwa ajili ya matibabu.

"Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, kwani inadaiwa mwanamke huyo alikuwa akimtuhumu mumewake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanawake wengine. Jeshi la Polisi linawakumbusha wananchi wote, hasa wanandoa, kutafuta suluhisho la migogoro kwa njia ya kisheria na ushauri wa kitaalamu kutoka kwa viongozi wa dini, wazazi, ustawi wa jamii na vyombo vya usuluhishi badala ya kujichukulia sheria mkononi na kusababisha madhara kwa watu wengine" imeeleza taarifa hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.