LIVE STREAM ADS

Header Ads

Amref Health Africa Tanzania Yakabidhi Vitendea Kazi Shinyanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Meneja wa Programu ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto kutoka Amref Health Africa nchini Tanzania, Dkt. Serafina Mkuwa (kulia) akikabidhi moja ya baiskeli maalum kwa ajili ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHWs) mkoani Shinyanga kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika la Amref Health Africa nchini Tanzania, kupitia mradi wake wa Thamini Uzazi Salama, limekabidhi vitendea kazi kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHWs) mkoani Shinyanga, kwa lengo la kuboresha huduma za afya ya uzazi kwa mama na mtoto, hasa katika maeneo ya vijijini na yaliyo pembezoni.

Vitendea kazi hivyo ni pamoja na baiskeli 56, makoti ya mvua, mabuti, fulana na mabegi ya kitaalamu, ambavyo vitawawezesha wahudumu hao kutoa huduma kwa ufanisi zaidi hata katika mazingira yenye changamoto za hali ya hewa na miundombinu.

Makabidhiano hayo yamefanyika Julai 1, 2025 katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, amelishukuru Shirika la Amref Tanzania kwa msaada wa vitendea kazi kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii, akibainisha kuwa vifaa hivyo vitaongeza ufanisi katika utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi.
"Serikali inatambua mchango wa wadau wa maendeleo, wakiwemo Amref Tanzania, katika kuhakikisha afya za wananchi hususan wanaoishi vijijini na maeneo ya pembezoni zinaimarika. Tutaendelea kushirikiana nao ili kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto," amesema Mhe. Mhita.

Aidha, ameeleza kuthamini juhudi za Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii katika kuhakikisha ustawi wa wananchi, hususan wanawake wajawazito na watoto wachanga.

"Tunatambua kazi kubwa inayofanywa na Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii, ikiwemo kufuatilia hali za wajawazito, kutoa elimu ya afya, kufanya rufaa na kukusanya taarifa muhimu za kiafya. Tunaamini vifaa hivi vitaongeza ufanisi wa kazi hiyo muhimu, kwa lengo la kupunguza vifo vya kina mama na watoto wachanga," ameongeza Mhe. Mhita.
"Serikali inatoa shukrani za dhati kwa wadau wetu  Amref Tanzania na Buffalo Bicycles Tanzania  kwa kuunga mkono jitihada za kuboresha afya ya uzazi, mama na mtoto. Tunawashukuru pia Serikali ya Canada kupitia Global Affairs Canada (GAC) kwa ufadhili, pamoja na UNFPA kwa usimamizi wa mradi huu. Vilevile, naipongeza timu nzima ya wasimamizi wa huduma za afya ngazi ya mkoa na halmashauri kwa ushirikiano mzuri katika utekelezaji wa shughuli hizi," ameongeza Mhe. Mhita.

Kwa upande wake, Meneja wa Programu ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto kutoka Amref Health Africa nchini Tanzania, Dkt. Serafina Mkuwa, ameeleza kuwa vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Thamini Uzazi Salama, unaofadhiliwa na Global Affairs Canada (GAC) na kusimamiwa na UNFPA.
Meneja wa Programu ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto kutoka Amref Health Africa nchini Tanzania, Dkt. Serafina Mkuwa akizungumza.

“Mradi huu unalenga kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga kwa kuboresha upatikanaji wa huduma salama za uzazi kupitia wakunga wenye ujuzi, vituo vya afya vilivyoimarika na wahudumu walioko karibu na jamii,” amesema Dkt. Mkuwa.

Ameongeza kuwa baiskeli hizo ni mchango kutoka Shirika la Buffalo Bicycles, ikiwa ni sehemu ya ushirikiano wa kimkakati wa kusaidia wahudumu wa afya kuwafikia wananchi kwa urahisi na haraka zaidi.

Meneja Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika la Buffalo Bicycles Rehema Richard amesema :“Tunaamini kuwa baiskeli bora ni daraja muhimu kwa mtoa huduma kufika kwa mlengwa kwa wakati. Kupitia ushirikiano huu na Amref, tunachangia mabadiliko ya kweli katika maisha ya Watanzania wengi.”

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, ameishukuru Amref Tanzania na wadau wake kwa msaada huo, akisisitiza umuhimu wa wahudumu kutumia vifaa hivyo kwa uadilifu:

“Naomba mtumie vifaa hivi kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuwafikia wananchi kwa wakati, kuimarisha huduma za afya ya uzazi, na kusaidia katika usajili wa kaya kwenye Bima ya Afya iliyoboreshwa”,amesema.
Wahudumu waliopokea vifaa hivyo tayari wamepatiwa mafunzo ya kutumia simu janja na programu ya LEAP, ambayo inawasaidia kupata elimu ya afya kwa njia ya kidijitali, kutoa elimu kwa jamii, kusaidia mfumo wa rufaa na kukusanya taarifa muhimu za kiafya.

Mradi wa Thamini Uzazi Salama unatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam na Shinyanga, ukilenga kuongeza idadi ya wakunga wenye ujuzi, kuimarisha huduma rafiki kwa mama na mtoto na kushirikisha jamii kwa kina katika matumizi ya huduma za afya ya uzazi kwa wakati.

Amref Health Africa inaendelea kushirikiana na Wizara ya Afya, TAMISEMI na wadau wengine kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata huduma bora za afya.

Kuboresha afya ya mama na mtoto na kuimarisha mifumo ya afya ya jamii ni msingi wa kujenga taifa lenye afya bora na ustawi endelevu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vitendea kazi kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHWs) mkoani Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la Amref Health Africa nchini Tanzania, kupitia mradi wake wa Thamini Uzazi Salama. Picha zote na Kadama Malunde
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vitendea kazi kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHWs) mkoani Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la Amref Health Africa nchini Tanzania, kupitia mradi wake wa Thamini Uzazi Salama.

Meneja wa Programu ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto kutoka Amref Health Africa nchini Tanzania, Dkt. Serafina Mkuwa akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vitendea kazi kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHWs) mkoani Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la Amref Health Africa nchini Tanzania, kupitia mradi wa Thamini Uzazi Salama.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vitendea kazi kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHWs) mkoani Shinyanga vilivyotolewa na Shirika la Amref Health Africa nchini Tanzania, kupitia mradi wa Thamini Uzazi Salama.
Meneja wa Programu ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto kutoka Amref Health Africa nchini Tanzania, Dkt. Serafina Mkuwa (kulia) akikabidhi moja ya baiskeli maalum kwa ajili ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHWs) mkoani Shinyanga kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita.
Meneja Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika la Buffalo Bicycles Rehema Richard akielezea kuhusu baiskeli maalum kwa ajili ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHWs) mkoani Shinyanga
Meneja Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika la Buffalo Bicycles Rehema Richard akielezea kuhusu baiskeli maalum kwa ajili ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHWs) mkoani Shinyanga.
Mmoja wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHWs) mkoani Shinyanga akipokea vitendea kazi
Meneja wa Programu ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto kutoka Amref Health Africa nchini Tanzania, Dkt. Serafina Mkuwa (kulia) akikabidhi vitendea kazi kwa ajili ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHWs) mkoani Shinyanga kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita.

No comments:

Powered by Blogger.