Shirika la EMEDO latoa mafunzo ya usalama kwa wavuvi
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la Mazingira na Maendeleo ya Kiuchumi (EMEDO) limetoa mafunzo kwa wavuvi 26 kutoka mwalo wa Sweya ulio katika mwambao wa Ziwa Victoria, jijini Mwanza.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Editrudith Lukanga alisema lengo ni kuwajengea uelewa wavuvi kujiokoa na kupeana huduma ya kwanza wakati wa dharura majini.
Pia Shirika hilo limekabidhi jaketi okozi (life jackets) 30 kwa Shirika la Uwaka wa Meli Tanzania (TASAC) ikiwa ni kuunga mkono jitihada za usalama majini ambapo jaketi hizo zimeelekezwa kutumika kwenye boti ya matibabu iliyowasili hivi karibuni jijini Mwanza.
Baadhi ya wavuvi walioshiriki mafunzo hayo akiwemo Emmanuel Joseph na Geas John waliomba Serikali kuondoa kodi kwenye vifaa okozi ikiwemo majaketi okozi hatua itakayosaidia kuuzwa kwa gharama nafuu.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda, Mkuu wa Wilaya ya Magu Amir Mkalipa alisema ombi la kutoa msamaha wa kodi kwenye vifaa okozi ziwani watalifikisha kwenye vikao vya maamuzi ili kufanyiwa kazi.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: