KIZA MAYEYE WA ACT WAZALENDO AJITOSA UBUNGE KIGOMA KASKAZINI
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kiza Mayeye wa ACT Wazalendo (kulia) akipokea fomu na nyaraka mbalimbali za kuomba uteuzi wa kugombea ubunge Jimbo la Kigoma Kaskazini kutoka kwa Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Linus Sikainda (kushoto).
***
Mwanamama Kiza Mayeye amechukua fomu ya uteuzi kutoka Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuwania ubunge Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kigoma Kaskazini, Linus Sikainda amesema Mayeye pamoja na wagombea wengine kutoka vyama 11 wamechukua fomu jana Jumatatu Agosti 25, 2025.
Sikainda ametaja vyama vingine ambavyo makada wake wamechukua fomu kufikia jana jioni kuwa ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ada Tadea, UDP, TLP, AAFP, DP, ADC, NLD, NRA na CUF.
Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu litahitimishwa kesho Agosti 27, 2025 na kufuatiwa na kampeni zinazotarajiwa kuanza Agosti 28, 2025.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: