LIVE STREAM ADS

Header Ads

TANESCO YAKAMATA WATU WATANO WAKIHUJUMU UMEME KAHAMA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Afisa Usalama wa TANESCO Mkoa wa Tabora na Msimamizi wa Usalama wa Kanda ya Magharibi, Said Sombwe, akionesha eneo ambalo wizi wa umeme ulikuwa ukifanyika wakati wa oparesheni maalum ya BAOMA wilayani Kahama.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewakamata watu watano katika Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, kwa tuhuma za matumizi haramu ya umeme katika oparesheni maalum iliyopewa jina la Baini Ajibisha Okoa Mapato (BAOMA).

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Agosti 29, 2025 Mhandisi Mkuu wa TANESCO Kanda ya Magharibi, Felix Mwinuka, amesema oparesheni hiyo imehusisha timu kutoka Makao Makuu, Kanda ya Kati na Kanda ya Magharibi kwa lengo la kuhakikisha mapato ya shirika hayapotei kupitia wizi wa umeme.
Mhandisi Mkuu wa TANESCO Kanda ya Magharibi, Felix Mwinuka

“Tumetembelea jumla ya wateja 473 na tumebaini wateja watano ambao walikutwa na matatizo mbalimbali. Baadhi walihamisha mita kinyume cha utaratibu, wengine walikuwa wanatumia umeme ambao haupiti kwenye mita – bypass na wapo waliochezea mita kinyume cha taratibu. Wote hawa tumewakabidhi kwenye vyombo vya dola kwa hatua za kisheria,” amesema Mwinuka.

Aidha, amewaonya wananchi kuacha vitendo vya kuhujumu miundombinu ya TANESCO akibainisha kuwa ni kosa la jinai na linaikosesha serikali mapato muhimu.

Kwa upande wake, Afisa Usalama wa TANESCO Mkoa wa Tabora na Msimamizi wa Usalama wa Kanda ya Magharibi, Said Sombwe, amesema lengo la ukaguzi ni kuhakikisha wateja wote wanatumia umeme kwa mujibu wa kanuni na taratibu.

“Tumejumuika kama timu kubwa kutoka makao makuu na kanda mbalimbali. Tumeweza kuwakamata wateja watano waliokuwa wanatumia umeme isivyo halali na tumewakabidhi vyombo vya kisheria. Rai yangu kwa wananchi ni kufuata taratibu za TANESCO kwa kuwa mkono wa shirika ni mrefu, tutawafikia popote,” amesisitiza Sombwe.
Omega Mathew Nyuki

Miongoni mwa waliokamatwa ni Omega Mathew Nyuki, mkazi wa Mhungula, ambaye amekiri kununua mita iliyohamishwa kinyume cha taratibu kutoka kwa mafundi wasio wa TANESCO ambapo gharama zote za kufikishiwa huduma alitoa Shilingi 650,000/=.

“Nilihitaji umeme baada ya kusitishiwa huduma. Mafundi wa mtaani waliniletea mita iliyohamishwa, nilijua wanatoka TANESCO maana huwa nawaona wanaunganisha huduma kwa wananchi, nikaikubali na nikaianza kutumia. Sikuwa na nia ya kuibia shirika, nilitafuta maisha yangu tu. Nimekamatwa na niko tayari kwa lolote litakalotokea,” amesema Nyuki kwa majonzi.

TANESCO imesema mbali na kutumia mita haramu, Nyuki alikuwa akiwauzia majirani zake huduma ya umeme kwa malipo ya Shilingi 100,000/-, hali iliyosababisha kusitishiwa huduma kwa wote aliowaunganishia.

Shirika hilo limeeleza kuwa oparesheni BAOMA itaendelea nchi nzima ili kuhakikisha wateja wote wanatumia umeme kwa mujibu wa sheria, na kuwataka wananchi kutoa taarifa za watu wanaohujumu miundombinu ya umeme.
Uunganishaji haramu wa nyaya uliofichuliwa na TANESCO katika oparesheni BAOMA, wilayani Kahama.
Sehemu ya mita iliyochezewa kwa ajili ya kuiba umeme, kama ilivyobainika katika oparesheni maalum ya TANESCO wilayani Kahama.
Afisa Usalama wa TANESCO Mkoa wa Tabora na Msimamizi wa Usalama wa Kanda ya Magharibi, Said Sombwe, akionesha eneo ambalo wizi wa umeme ulikuwa ukifanyika wakati wa oparesheni maalum ya BAOMA wilayani Kahama.
Afisa Usalama wa TANESCO Mkoa wa Tabora na Msimamizi wa Usalama wa Kanda ya Magharibi, Said Sombwe, akionesha eneo ambalo wizi wa umeme ulikuwa ukifanyika wakati wa oparesheni maalum ya BAOMA wilayani Kahama.
Afisa Usalama wa TANESCO Mkoa wa Tabora na Msimamizi wa Usalama wa Kanda ya Magharibi, Said Sombwe, akionesha eneo ambalo wizi wa umeme ulikuwa ukifanyika wakati wa oparesheni maalum ya BAOMA wilayani Kahama.
Afisa Usalama wa TANESCO Mkoa wa Tabora na Msimamizi wa Usalama wa Kanda ya Magharibi, Said Sombwe akizungumza wakati wa oparesheni maalum ya BAOMA wilayani Kahama.
Afisa Usalama wa TANESCO Mkoa wa Tabora na Msimamizi wa Usalama wa Kanda ya Magharibi, Said Sombwe akizungumza wakati wa oparesheni maalum ya BAOMA wilayani Kahama.
Mhandisi Mkuu wa TANESCO Kanda ya Magharibi, Felix Mwinuka akizungumza wakati wa oparesheni maalum ya BAOMA wilayani Kahama.
Omega Mathew Nyuki, mkazi wa Mhungula, ambaye amekiri kununua mita iliyohamishwa kinyume cha taratibu kutoka kwa mafundi wasio wa TANESCO.

No comments:

Powered by Blogger.