MATEMBEZI YA PAMOJA YA VYOMBO VYA USALAMA MWANZA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Leo Ijumaa tarehe 10 Oktoba 2025, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limeendelea na matembezi ya pamoja (Route March) yenye umbali wa zaidi ya kilomita 7 yaliyoanzia uwanja wa Polisi Mabatini na kupita mitaa mbalimbali.
Mazoezi hayo yameshirikisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji, Polisi Wasaidizi na Mgambo, kwa lengo la kuimarisha afya, nidhamu, mshikamano na utayari wa utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi SACP Gideon Msuya amewapongeza askari kwa kujitoa kikamilifu wakati wote wa mazoezi, akisisitiza umuhimu wa kuendeleza mshikamano katika kulinda usalama wa wananchi na mali zao.
Kutoka Dawati la Habari Polisi Mwanza
No comments: